TRA

TRA

Friday, March 3, 2017

Paa laporomoka hospitali ya umma Afrika Kusini

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !
Paa la hospitali moja ya umma nchini Afrika Kusini limeanguka na kujeruhi watu kadhaa. Wagonjwa na wafanyakazi katika hospitali ya Charlotte Mexeke mjini Johannesburg walikwama ndani ya jengo baada ya paa lake kuporomoka wakati mafundi ujenzi wakijaribu kuziba sehemu iliokuwa inavuja. Watu wasiopungua watano walipata majeraha, na haikubainika mara moja wangapi walikuwa wamekwama katika jengo hilo. Picha za TV zilionyesha waokoaji wakiondoa vifusi katika juhudi za kuwafikia watu waliokwama ndani ya hospitali hiyo. Maafisa wamesema tukio hilo linamulika tatizo la uhaba wa ufadhili unaoukabili mfumo wa sekta ya afya ya umma nchini Afrika Kusini.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger