TRA

TRA

Friday, March 3, 2017

Sweden yaanzisha upya utumishi wa lazima jeshini

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !
Wizara ya ulinzi ya Sweden jana imetangaza kurejesha mpango wa utumishi wa laazima jeshini, mnamo wakati wasiwasi unaongezeka kuhusu vitendo vya Urusi nchini Ukraine. Sweden iliufuta mpango huo mwaka 2010, lakini mizozo ya kikanda imeilaazimu serikali kwa mara nyingine kuandikisha vijana kwa ajili ya mafunzo ya kijeshi. Uandikishaji wanajeshi utaanza rasmi mwaka 2018, na utajumlisha watu waliozaliwa mwaka 1999 au baada ya hapo, ambapo karibu watu 13,000 wametakiwa kuripoti kwenye usaili, na 4000 watachaguliwa kwa ajili ya mafunzo. Uandikishaji huo utahusisha wanawake, ambao tayari wanachangia hadi asilimia 16 ya jeshi la Sweden lenye jumla ya watu 20,000.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger