TRA

TRA

Tuesday, March 21, 2017

Rais wa zamani wa Korea Kusini ahojiwa

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !
Rais wa Korea Kusini aliyeondolewa madarakani Park Guen-Hye amehojiwa na waendesha mashitaka leo kuhusu kashfa ya rushwa na matumizi mabaya ya madaraka iliyomuangusha. 

Park amehojiwa baada ya kutumia mamlaka yake kuwakwepa waendesha mashitaka kwa miezi kadhaa wakati alipokuwa madarakani. 

Amewaomba radhi wananchi lakini akakanusha kufanya makosa wakati alipowasili katika ofisi za waendesha mashitaka mjini Seoul na kuahidi kushirikiana kikamilifu katika uchunguzi huo. 

Rais huyo wa kwanza mwanamke wa Korea Kusini aliondolewa na bunge Desemba mwaka uliopita wakati mamilioni ya watu walipoandamana barabarani kumtaka ajiuzulu kutokana na kashfa hiyo. 

Park huenda akakabiliwa na mashitaka ya uhalifu na kufungwa jela kwa miaka 10 iwapo atatiwa hatiani.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger