TRA

TRA

Tuesday, March 21, 2017

Marekani yakataza vifaa vya kielektroniki katika ndege

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !
Marekani imepiga marufuku kwa muda vifaa vikubwa vya kielektoniki kama kompyuta za kupakata, kamera, iPads visiingizwe katika mizigo inayobebwa na abiria ndani ya ndege kutoka mataifa kadhaa ya Mashariki ya Kati. 

Sababu ya marufuku hiyo haikufahamika mara moja na maafisa wa Marekani hawakutaka kusema chochote. Taarifa iliyotumwa katika mtandao wa Twitter na shirika la ndege la Saudi Airlines na taarifa iliyofutwa ya shirika la Royal Jordanian ziliwafahamisha wateja wao kuhusu marufuku hiyo ya vifaa vya kielektroniki vilivyo vikubwa kuliko simu ya mkononi.

Shirika la Royal Jordanian lilisema vifaa kama kompyta aina ya laptop, kamera na vifaa vya kuchezea DVD na michezo ya kielektoniki vitahitaji kuchunguzwa chini ya sheria mpya za serikali ya Marekani zinazoanza kutekelezwa leo. Simu za mkono na vifaa vya utabibu vinavyohitajika ndani ya ndege vitaruhusiwa.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger