Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (Kushoto) akizungumza na Ujumbe
kutoka Jamuhuri ya watu wa China pamoja na baadhi ya Watumishi wa Wizara
yake (hawapo katika picha) wakati wa hafla ya kusaini Mkataba wa
programu ya Utekelezaji wa masuala ya Utamaduni baina ya Tanzania na
China wa miaka mitatu kuanzia mwaka 2017 hadi 2020 iliyofanyika leo
Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Waziri wa Utamaduni Jamhuri ya watu
wa China Mhe. DONG WEI.
Naibu Waziri wa Utamaduni Jamhuri
ya watu wa China Mhe. DONG WEI akitoa maelezo mafupi kwa Ujumbe wa
Serikali ya China pamoja na baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Habari
(hawapo katika picha) katika hafla ya kusaini Mkataba wa programu ya
Utekelezaji wa masuala ya Utamaduni baina ya Tanzania na China wa miaka
mitatu kuanzia mwaka 2017 hadi 2020 iliyofanyika leo Jijini Dar es
Salaam. Katikati ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.
Nape Moses Nnauye na kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof.
Elisante Ole Gabariel.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (aliyekaa kushoto) pamoja na Naibu
Waziri wa Utamaduni wa China Mhe. DONG WEI (aliyekaa kulia) wakisaini
Mkataba wa programu ya utekelezaji wa masuala ya Utamaduni baina ya
Tanzania na China wa miaka mitatu kuanzia mwaka 2017 hadi 2020
iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Katikati aliyesimama ni Katibu
Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole
Gabariel.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (Kushoto) pamoja na Naibu Waziri wa
Utamaduni wa China Mhe. DONG WEI (kulia) wakikabidhiana Mkataba wa
programu ya Utekelezaji wa masuala ya Utamaduni baina ya Tanzania na
China wa miaka mitatu kuanzia mwaka 2017 hadi 2020 iliyofanyika leo
Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (Kushoto) akimkabidhi zawadi ya
Kinyago Naibu Waziri wa Utamaduni kutoka Jamuhuri ya watu wa China Mhe.
DONG WEI (kulia) mara baada ya kusaini Mkataba wa programu ya
Utekelezaji wa masuala ya Utamaduni baina ya Tanzania na China wa miaka
mitatu kuanzia mwaka 2017 hadi 2020 iliyofanyika leo Jijini Dar es
Salaam.
Picha na: Genofeva Matemu – WHUSM
……….
Na Shamimu Nyaki-WHUSM.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye pamoja na Naibu Waziri wa Utamaduni
kutoka Jamhuri ya watu wa China Mhe. DONG WEI wamesaini programu ya
utekelezaji wa Mkataba wa masuala ya Utamaduni wa miaka mitatu kuanzia
mwaka 2017 hadi 2020 leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri Nape ameeleza kuwa Mkataba
huo unalengo la kuimarisha na kuendeleza ushirikiano katika Sekta ya
Utamaduni ambao umedumu kwa miaka mingi ulioasisiwa na Baba wa Taifa
Mwl.Julius K. Nyerere.
“Tanzania na China tumekuwa na
ushirikiano wa muda mrefu wa masuala mbalimbali ikiwemo hili la
Utamaduni ambalo limetumika kukuza, kulinda na kuunganisha nchi zetu
kuwa kitu kimoja”, Alisema Mhe. Waziri.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa
Utamaduni wa China Mhe. DONG WEI amesema kuwa ushirikiano kati ya
Tanzania na China uliokuwepo kwa muda mrefu katika masuala ya
Utamaduni, Sanaa, Elimu,Ngoma na Michezo yamesaidia kuimarisha
ushirikiano uliopo na kuwezesha nchi hizi mbili kunufaisha katika maeneo
hayo.
“Ushirikiano wetu wa muda mrefu
katika masuala ya Utamaduni umeleta mafanikio makubwa ambayo sote
tunajivunia kila tunapokuwa pamoja”.Alisema Mhe. WEI.
Mkataba huo pamoja na mambo
mengine una lengo la kuendeleza na kufanya mpango wa pamoja kwa siku za
usoni, kufanya matokeo makubwa katika Sekta ya Utamaduni kati ya nchi
hizo mbili, Kufanya mkutano maalum wa ushirikiano wakati muafaka,
kuzidisha ushirikiano kwenye sekta ya viwanda katika bidhaa za Utamaduni
na Kubadilishana wataalamu na mafunzo ya kiutamaduni.
Katika hatua nyingine Serikali
hiyo ya China imeisaidia Wizara kiasi cha Yuan laki nne (400,000) kwa
ajili ya kununua vifaa mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya Wizara.
SHARE
No comments:
Post a Comment