TRA

TRA

Thursday, March 2, 2017

SERIKALI YAKOMAA NA OPERESHENI YA VIROBA

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !
 



Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 

Operesheni ya kukagua pombe zinazofungashwa kwenye vifungashio vya Plastiki (Viroba) ambapo jana katika manispaa ya Temeke na Kinondoni wamefunga viwanda na maghala kutoendelea na uzalishaji ,kuuza wala kusambaza. 

kiwanda cha Global Distillers Limited watengenezaji wa pombe kali aina ya viroba aina ya Premium Vodka na Ginja ambapo walifanikiwa kukamata katoni 1500 na ghala ambalo lilikutwa na katoni 650 na Wilaya ya Kinondoni na Ubungo kiwanda cha Kibo Spirit na True Bell navyo vilizuiwa uzalishaji baada ya kukuta pombe hiyo ya viroba ikiwa imesheheni aina ya Kitoko na Rivella Vodka kimakosa. 

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ukaguzi huo kwa upande wa Wilaya Kinondoni na Ubungo Mwanasheria wa Baraza la Mazingira (NEMC ) Heche Suguta amesema operesheni hiyo endelevu lengo ni kuhakikisha agizo laserikali linatekelezeka kwa wafanyabiashara hao kusitisha utengenezaji wa vileo katika vifuko ‘ viroba’. 

Amesema wanafunga na kusitisha uzalishaji huo hadi hapo utaratibu mwingine utakapofuatwa ikiwa ni pamoja na kutumia teknolojia mpya.
Amesema lengo ni kusimamisha uzalishaji na hata uingizwaji kwa kuwa vileo vingine vinatoka nje ya nchi na aliongeza kuwa hata kwa wale wa mpakani tayari wameshawasiliana na Jeshi la Polisi kuhakikisha wanazuia uingizwaji na kama mtu amekamatwa basi anatakiwa mzigo wake urudishwe ulipotoka. 

Katika manispaa ya Kinondoni pia ukaguzi ulifanyika katika maghala mbalimbali ikiwemo la Triple S Investment Company Ltd na muhusika kukimbia ambapo timu ya ukaguzi ilikuta makufuli yakiwa yamefunguliwa na jengo zima kutokuwa na mtu. 

Katika ghala hilo pia ambalo muhusika alikimbia walikutana na vifungashio kwa nje aina ya Signal true Vodka ujazo asilimia 100.Katika ghala la Kibo Sprit uongozi wa hapo walisema hawajaanza uzalishaji zaidi ya kuwa na ghala hilo na upande Temeke ,Kiongozi wa msafara katika timu hiyo Mkaguzi kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Aron Nzalla alisema ukaguzi wameufanya kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama. 

Katika ukaguzi wa kiwanda cha Global distillers mkaguzi huyo alimweka chini ya ulinzi wafanyakazi wa kampuni hiyo akiwemo mhasibu ,Ofisi Ugavi na Manunuzi pamoja na mlinzi (majina yamehifadhiwa ).


Mwanasheria toka Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Bw. Manchare Heche (kushoto) akikagua nyaraka toka kwa Msimamizi wa Kiwanda cha True Bell (T) Limited Bw. Godwin Mungere mapema leo hii jijini Dar es Salaam wakati wa siku ya pili ya operesheni ya kusaka wasambazaji wa kinywaji hicho ambacho Serikali imepiga marufuku kutumika.
Baadhi ya Maafisa wa Serikali wakikagua ghala la Kiwanda cha True Bell (T) Limited mapema hii leo Jijini Dar es Salaam wakati wa siku ya pili ya operesheni ya kusaka wasambazaji wa kinywaji hicho ambacho Serikali imepiga marufuku kutumika.
Msimamizi wa Kiwanda cha True Bell (T) Limited Bw. Godwin Mungere (mwenye shati la njano) akionesha baadhi ya vifungashio vya pombe kali aina ya kiroba mapema hii leo Jijini Dar es Salaam wakati wa siku ya pili ya operesheni ya kusaka wasambazaji wa kinywaji hicho ambacho Serikali imepiga marufuku kutumika, kulia ni Mwanasheria toka Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Bw. Manchare Heche
Baadhi ya shehena ya maboksi ya pombe ya viroba aina ya bonanza ikiwa imehifadhiwa katika ghala la kiwanda cha True Bell (T) Limited kilichopo Sinza Bamaga mapema leo hii jijini Dar es Salaam wakati wa siku ya pili ya operesheni ya kusaka wasambazaji wa kinywaji hicho ambacho Serikali imepiga marufuku kutumika.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger