Na Anna Nkinda – JKCI
14/3/2017
Jumla ya wagonjwa 11 wamefanyiwa upasuaji wa moyo katika kambi maalum
ya matibabu ya moyo inayofanywa na madaktari bingwa wa upasuaji wa moyo
kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ushirikiana na
madaktari wenzao wa Taasisi ya Open Heart International ya nchini
Australia.
Hayo
yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Upasuaji wa Moyo ambaye pia ni Daktari
bingwa wa upasuaji wa Moyo Bashir Nyangasa wakati akielezea jinsi kambi
hiyo ya upasuaji inavyoendelea kutoa matibabu kwa wagonjwa.
Dkt.
Nyangasa alisema, “Kwa kushirikiana na washirika wetu wa OHI tulianza
kambi maalum ya upasuaji kuanzia tarehe 10/03/2017 hadi leo tarehe 17/3/2017 tumefanya upasuaji kwa wagonjwa 11 ambao wanaendelea vizuri, kati ya hao watoto ni tisa na watu wazima ni wawili”,.
Dkt. Nyangasa alisema katika kambi hiyo ambayo inamalizika tarehe 17/3/2017 walipanga kufanya upasuaji kwa wagonjwa 25 kati ya hao watoto ni 15 na watu wazima ni 10.
Kuhusu uhitaji wa
damu kwa wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji wa Moyo Dkt. Nyangasa alisema
wagonjwa hao wanahitaji damu nyingi hivyo basi aliwaomba wananchi wajitokeze kuchangia damu ambayo itatumika kwa wagonjwa.
“Tunaomba wananchi wajitokeze kwa wingi kuchangia damu na uchangiaji huu wa damu usifanyike mara moja bali uwe endelevu kwani
Taasisi inatoa huduma kwa wagonjwa wakati wote siyo wakati wa kambi
maalum za matibabu ya moyo pekee yake”, alisisitiza Dkt. Nyangasa.
Tangu kuanza kwa mwaka huu wa 2017 JKCI kwa kushirikiana na baadhi ya washirika wake wa nje ya nchi ambao ni Madaktari Afrika wa Marekani, Hospitali za Apolo Bangalore na BLK zote za nchini India na Open Heart International ya Australia wamefanya matibabu ya moyo ya kufungua na bila kufungua kifua kwa wagonjwa wa moyo wanaotibiwa katika Taasisi hiyo.
SHARE
No comments:
Post a Comment