Mashirika
na asasi zote ambazo hazikumbatii na kukubali mfumo wa kuendesha
biashara kidigitali zinajiweka pabaya kutemwa na wateja wao.
Kutokana
na tishio hili, Telkom and Business Connexion inazindua rasmi BCX,
mfumo mpya na wa kisasa kidigitali unaoongoza barani Afrika, unaotumika
kurahisisha mawasiliano ya miamala ya biashara na mawasiliano.
Toleo
hili jipya la teknolojia, lililoandaliwa kwa ushirika kati ya Telkom
Business na Business Connexion, ni la kipekee katika ufumbuzi wa
kitekinolojia unaosambaa kwa kasi barani Afrika kuwezesha na kurahisisha
mawasiliano na ufanisi wa kibiashara.
“Uzinduzi
wa BCX kwa kweli unafungua ukurasa mpya katika mwelekeo wa ufanisi wa
kibiashara kwa tekinoljia pevu barani Afrika,” alisema Seronga Wangwe
ambaye ni Mkurugenzi wa BCX Tanzania, katika hotuba yake ya ufunguzi
aliyoitoa hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency, jijini Dar Es Salaam.
“BCX
imejengwa kutoka katika msingi imara wa Telkom Business yenye maarifa
na elimu pevu ya miundombinu ya mawasiliano pamoja na taaluma ya
muunganisho wa kibiashara inayojali kutoa huduma kwa ukaribu na
unyenyekevu kwa wateja wake.
“BCX sasa ni bidhaa mpya ya mawasiliano barani Afrika yenye ufanisi wa kutoa huduma kwa umakini mkubwa’, aliongeza Bwana Wangwe.
Mfumo
wa kidigitali uliopevuka unapewa kipaumbele na aina zote za biashara
barani Afrika. Kwa sasa inaelewaka bayana kuwa kampuni yeyote ambayo
inakwepa au kudharau kuendesha miamala yake kidigitali ipo hatarini
kutorokwa na wateja katika mwelekeo wa kudorora kabisa!
BCX
inatoa mwelekeo mpya popote barani Afrika katika kutoa huduma
kidigitali ili kutoa huduma bora kibiashara kwa sasa na kwa muda mrefu
kwa wateja wake.
“Hakuna kitu kilichonifurahisha zaidi leo hii kama uzinduzi huu mpya wa BCX,” alisema, mkuu wa BCX international ALTHON BEUKES.
BCX
inaweka bayana aina ya mawasiliano na mahitaji yote ya makampuni
yaliyomo barani Afrika katika kutoa ufumbuzi sahihi wa matatizo ya
mawasiliano kibiashara, katika masoko yake ya ndani na hatimaye kupenya
nje ya mipaka na kusambaa barani kote. Itasawazisha uwezo wa makampuni
katika kujitanua kitekinolojia na mahitaji ya mawasiliano ya makampuni
barani Afrika.
“BCX’s
imetandaza nyayo zake kibiashara barani Afrika ikiwa na makampuni tanzu
katika nchi kama vile Kenya, Nigeria, Tanzania, Namibia, Zambia na
Botswana, halikadhalika uwepo wake huko Dubai na Uingereza, inatufanya
tuwe mfano pekee na bora kwa mwasiliano na washirika na wateja wetu wote
wanaofanya biashara nasi barani Afrika na wale walio katika matarajio
ya kujiunga nasi katika mwelekeo wa ufanisi kibiashara ili kuliongoza
bara la Afrika kwenye ushindi wa nafasi za kibiashara,” aliongeza.
Uzinduzi
wa BCX ni hatua ya mwisho katika kunyumbulisha Telkom Business na
Business Connexion. BCX itaendelea kujikita ndani ya Telkom Group,
lakini itajali kufanya biashara katika ufanisi mkubwa. Wafanyakazi wote
wanafahamu umuhimu wa tekinolojia hii mpya na ofisi zote zina thamini
bidhaa hii mpya ya mawasiliano. Kwa kuongozea, miamala yote ya
kibiashara na wateja itajikita katika sura mpya ya utambulisho wa BCX.
BCX
kwa kwenda mbele itaendelea kuangalia kwa umakini mahitaji ya wateja
wake na kutoa ufumbuzi wa uhakika hususan kwa matumizi ya kompyuta,
mawasiliano na ushirikainao wa karibu, na mnyumbulisdho wa kibiashara
wenye usalama wa uhakika kwa mtandao pamoja na uchambuzi makini wa
takwimu za kibiashara.
Mkurugenzi
mtendaji wa kampuni ya BCX Tanzania Bw. Seronga Wangwe (kushoto)
akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam katika uzinduzi wa
kampuni ya BCX ambayo imejumuisha kampuni za Business connexion na
Telkom katika hafla fupi iliyofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency,
Kulia ni meneja mauzo wa kampuni hiyo Bw. Ebenezer Massawe.
Kutoka kushoto ni Bwa. Seronga Wangwe, (mwakilishi) kutoka Mozambique High Commission, Bwa.Frans Van Aardt- Councelor kutoka ubalozi wa Afrika kusin,Bi.Monica Patricio Clemente- Balozi wa Msumbiji, pamoja na Bwa.Althon Beukes- mkuu wa BCX International wakiwa katika picha ya pamoja.
. Mgeni rasmi Bw. Frans Van Aardt ambaye ni Councelor wa Ubalozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania. Akizungumza katika Uzinduzi wa kampuni ya BCX uliofanyika Hyatt hotel Dar es salaam
Mkuu wa BCX International Bw. Althon Beukes akizungumza na wageni katika hafla fupi ya uzinduzi wa kampuni ya BCX, iliyofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es salaam
Wasanii kutoka kikundi cha Kigamboni Community Centre (KCC) wakitoa burudani ya ngoma za asili kwa wageni na waalikwa katika siku ya uzinduzi wa kampuni ya BCX nchini Tanzania uliofanyika katika hoteli ya Hyatt regency (the Kilimanjaro).
Wageni mbalimbali waliohudhuria katika hafla ya uzinduzi wa BCX Tanzania
Bw.
Seronga Wangwe (Mkurugenzi mtendaji wa BCX Tanzania) akizungumza na
wageni waalikwa katika hafla fupi ya uzinduzi wa kampuni hiyo siku ya
jumatano katika hoteli ya Hyatt Regency Dar es salaam
SHARE
No comments:
Post a Comment