Rais wa Marekani Donald Trump amedai kura ya kuukubali ama kuukataa muswada mpya wa afya ipigwe Ijumaa katika bunge la wawakilishi.
Muswada huo mpya wa afya unalenga kubadilisha baadhi ya sehemu ya sheria iliyosainiwa na rais Barack Obama.Lakini upigaji kura ulicheleweshwa siku ya Alhamisi kutokana na upinzani kutoka kwa baadhi ya wabunge wa Republican - licha ya majaribio ya mara kwa mara ya bwana Trump ya kuwashawishi wauunge mkono muswada huo.
Kwa sasa anasema anataka upigiwe kura Ijumaa kwa vyovyote vile matokeo yatakayotokea.
Mkurugenzi wa bajeti ya Ikulu ya White House Bwana Mick Mulvaney amesema huu ndio ujumbe uliofikishwa kwa wabunge wa Republican katika mkutano wa faragha uliofanyika Alhamis.
"Kwa miaka saba na nusu tumekuwa tukiwaahidi watu waMarekani kwamba tutarekebisha na tutabadilisha sheria hii mbaya kwa sababu haifai familia za waMarekani, na kesho tunafanya hivyo," alisema Spika wa bunge Paul Ryan .
" kama kwa sababu yoyote haitachaguliwa, tutaendelea na nyongeza za sehemu ya agenda yake."
Kuondoa mpango wa bima ya matibabu ijulikanayo kama Obamacare ilikuwa ndiyo kauli mbiu ya Bwana Trump wakati wa kampeni zake za uchaguzi.
Kuahirishwa kwa upigaji kura jana Alhamisi lilikuwa ni pigo kwa rais Trump ambaye alisisitiza kuwa atapata uungaji mkono wa idadi kubwa ya wabunge watakaopitisha muswada huo katika bunge la wawakilishi siku hiyo.
Mapema siku ya Alhamis, Kiongozi wa walio wachache bungeni Nancy Pelosi alisema kuwa ''Trump alifanya kosa kwa kuleta bungeni muswada huu katika siku ambapo anafahamu fika kuwa anajua hauko tayari''
Muswada huo unahitaji kura 215 kuweza kuidhinishwa, lakini ulikabiliwa na upinzani hususan kutoka kwa wabunge wa Republican wenye misimamo mikali wanaoamini kuwa haukuandaliwa ipasavyo kiasi cha kuipiku sheria ya Bwana Obama iliyolenga kutoa matibabu kwa gharama nafuu.
SHARE
No comments:
Post a Comment