TRA

TRA

Wednesday, March 22, 2017

VIDEO:Gwajima atembelea Clouds media, asema yeye amekuwa mwanafamilia wa Clouds

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !




Mchungaji wa kanisa la ufufuo na uzima, Josephat Gwajima amewasili ofisi za clouds media kama alivyoahidi. Kuwa pamoja nami nikujuze kinachojiri.
=======



Kiongozi huyo wa kanisa la ufufuo na uzima amefika katika ofisi hizo saa 4:00 asubuhi akiwa na msafara wa magari zaidi ya manne huku yeye akiwa kwenye gari aina ya Hammer na kupokelewa na mwenyeji wake Ruge Mutahaba. Gwajima amesema ameenda Clouds kwa sababu yeye ni sehemu ya stori na hio sio stori ya kisiasa. Amedai clouds wamefanya huo ufafanuzi kwa nia njema, kutaka kuombwa radhi na mtu mmoja alietumia madaraka yake vibaya na sio serikali.

Swali(Mtanzania): Kwanini unafikiri wewe ni chanzo?

Jibu(Gwajima): Jina langu lilikuwa miongini mwa yaliyotajwa na nikiwa kiongozi wa dini pekee. Sijawahi kutumia kilevi cha aina yeyeto, walifanya uchunguzi wa madawa na money laundering hawakunikuta na hatia. Nilipofatilia inawezekanaje mtu akataja watu bila ushahidi nikagundua ndugu yetu hakumaliza elimu.

Watu wengi wamepoteza nafasi zao kwa ajili ya vyeti ikiwemo wanafunzi na wafanyakazi, inakuwaje mtu mmoja yeye ameachwa.

Swali(Global): Inasemekana wewe na mkuu wa mkoa mna interest ya jimbo moja

Jibu: Naita ni kuogopa tembo ambae hajazaliwa, Kolomije ambayo ipo jimbo la Misungwi ni nyumbani kwetu na sina nia ya nia ya jimbo, kuogopa kitu ambacho hakipo hakina maana sana kwa ambae amesoma, inayeogopa una-question shule yake. Nina watoto watatu, sina mtoto mwingine na hata angekuwepo ningelea lakini siwezi kulea mtoto ambae sio wangu.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger