Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Ashatu Kijaji (Mb) akisisitiza kuhusu
jitihada zinazofanywa na Serikali katika kutatua changamoto ya deni la
Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco) kwa kuendeleza juhudi za
kutumia nishati mbadala ya Gesi badala ya Mafuta mazito katika kuendesha
mitambo ya Uzalishaji wa umeme, katika kikao na Wakurugenzi Watendaji
wanaoziwakilisha nchi zao katika Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB),
ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.
Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb)(kushoto)
akiongoza Mkutano wa Wakurugenzi Watendaji wanaoziwakilisha nchi zao
katika Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), katika kufanya tathmini ya
maendeleo ya Miradi inayofadhiliwa na Benki hiyo, ambapo Wakurugenzi hao
waliipongeza Tanzania kwa kutekeleza miradi kwa ufanisi. Kulia ni
Mkurugenzi Mtendaji kutoka Afrika ya Kusini Bi. Mmakgoshi Lekhethe
aliyeongoza ujumbe wa Wakurugenzi Watendaji wengine 12 (hawapo pichani),
katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, jijini Dar es Salaam.
Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kushoto) na
Mkurugenzi Mtendaji kutoka Afrika ya Kusini Bi. Mmakgoshi Lekhethe
(kulia) wakipeana mikono baada ya kumalizika kwa mkutano wa tathmini ya
maendeleo ya Miradi inayofadhiliwa na Benki hiyo nchini Tanzania, katika
ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.
Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (wanne kulia)
na Mkurugenzi Mtendaji kutoka Afrika ya Kusini Bi. Mmakgoshi Lekhethe
(wa tano kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi Watendaji
wanao ziwakilisha nchi zao katika Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB),
baada ya kumalizika kwa mkutano wa tathmini ya maendeleo ya Miradi
inayofadhiliwa na Benki hiyo nchini Tanzania, katika ukumbi wa Wizara ya
Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.
Mmoja
wa Wakalimani aliyeambatana na Wakurugenzi Watendaji wanao ziwakilisha
nchi zao katika Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), akisalimiana kwa
bashasha na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji
(Mb), (kulia) baada ya kumalizika kwa mkutano wa tathmini ya utekelezaji
wa miradi inayofadhiliwa na Benki hiyo nchini Tanzania, katika ukumbi
wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es salaam, ikiwa ni ishara
njema kwa Taifa kwa kuwa walipongeza jitihada zinazofanywa na Serikali
za kupambana na umaskini.
Na Benny Mwaipaja, WFM
Naibu
Waziri Wizara ya Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) amesema
Serikali inaendelea kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB)
katika kuhakikisha miradi yote ikiwemo ile inayofadhiliwa na Benki hiyo
inatekelezeka kwa ufanisi Mkubwa.
Dkt.
Kijaji ameyasema hayo alipokutana na Wakurugenzi Watendaji 12
wanaoziwakilisha nchi zao katika Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB),
katika Mkutano uliofanyika Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es
salaam, baada ya ujumbe huo kutembelea miradi mbalimbali inayofadhiliwa
na Benki hiyo hapa nchini.
“Madhumuni
makubwa ya ziara ya Wakurugenzi watendaji wa Benki ya AfDB waliokuja
nchini tangu Februari 25, ni kukaa pamoja na Serikali ili kujadiliana
kuhusu sera na mipango mikakati ya maendeleo, lakini pia kutembelea
miradi mbalimbali inayotekelezwa kupitia ufadhili wa Benki ya hiyo”
Alifafanua Dkt. Kijaji.
Wakurugenzi
hao ambao ndio watoa maamuzi katika Benki hiyo, wametembelea miradi ya
maji Zanzibar na kwa upande wa Tanzania Bara wametembelea mradi wa kufua
umeme wa Sokoine substation uliopo Manispaa ya Ilala.
Katika
Mkutano huo, Serikali ya Tanzania imeendelea kuiomba Benki ya AfDB
kuharakisha kazi za upembuzi yakinifu na hatimaye kutoa fedha ili
utekelezaji wa miradi ya Maendeleo uanze mapema kwa kadri
inavyowezekana.
Miradi
hiyo ni pamoja na ule wa North – West grid wa kusafirisha Nishati ya
Umeme kutoka Shinyanga hadi Mbeya kupitia Kigoma Katavi na Rukwa. Mradi
utakaowezesha Mikoa ya Ukanda wa Magharibi kupata Nishati ya uhakika ya
umeme na kufungua fursa za Maendeleo mbalimbali yakiwemo ya ujenzi wa
Viwanda vidogo na vya kati.
Kwa
kushirikiana na Benki hiyo ya AfDB mradi mwingine unaofanyiwa kazi ili
kupata fedha za kuanza kuutekeleza ni ule wa kujenga barabara ya
Nyakanazi, kupitia Kibondo, Kasulu hadi Manyovu, kwa kiwango cha lami na
iwapo mradi huo ukipatiwa fedha na kukamilika kwa wakati kutasaidia
kuchochea biashara ya wakazi wa maeneo hayo pamoja na Nchi ya Burundi.
Kwa
upande wa Wakurugenzi Watendaji wa AfDB wanaoziwakilisha nchi zao,
wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji kutoka Afrika ya Kusini Bi. Mmakgoshi
Lekhethe, wameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John
Pombe Joseph Magufuli kwa ufanisi katika Nyanja zote ikiwemo ya
kupambana na umaskini.
Wageni
hao wamefurahishwa na namna Tanzania invyotekeleza miradi
inayofadhiliwa na Benki hiyo, kwa kuwa kila walipopatembelea, wameona
uthabiti na umadhubuti wa miradi, jambo ambalo limewaongezea hamasa ya
kufanya kazi kwa karibu na nchi hiyo.
Wameitaka
Serikali kuendelea kulishughurikia suala la deni la Shirika la Ugavi wa
Umeme Tanzania-TANESCO, ili kuongeza ufanisi wa kiutendaji kwa lengo la
kuchochea maendeleo ya nchi mijini na Vijijini.
Naibu
Waziri Dkt. Kijaji amebainisha kuwa ipo mikakati iliyowekwa na Serikali
ya kutatua suala la deni hilo kwa kuwa tatizo kubwa lilikuwa matumizi ya
Mafuta ya dizeli katika kuendeshea mitambo TANESCO.
Aidha
alisema kuwa kwa sasa upatikanaji wa Nishati ya Gesi katika maeneo
mbalimbali ya Tanzania, utasaidia katika kuendesha mitambo hiyo badala
ya Mafuta hivyo kutatua suala la deni hilo linalo likabili Shirika na
hatimaye kutimiza ndoto ya watanzania ya kuimarika kwa uchumi utakao
chochewa na Sekta hiyo.
SHARE
No comments:
Post a Comment