TRA

TRA

Saturday, March 4, 2017

Wanajeshi mbaroni Sudan Kusini kwa ubakaji

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !
Wanajeshi watatu wamekamatwa nchini Sudan Kusini kwa tuhuma za ubakaji. Msemaji wa kijeshi ameeleza kwamba tukio hilo lilitokea nje ya mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba ambako viongozi wa kijamii waliripoti kwamba wanawake wasiopungua 10 pamoja na mtoto mmoja walibakwa na kuteswa. Hatua hii imetokana na ahadi ya rais Salva Kiir ya kuwafikisha mbele ya sheria, wanajeshi waliofanya vitendo vya ubakaji na dhulma za kingono dhidi ya raia. Inaaminika maelfu ya wanawake na wasichana walibakwa nchini Sudan Kusini ambayo haina utulivu, baada ya kuzuka kwa mgogoro wa kijeshi kati ya rais Kiir na makamu wake wa zamani Riek Machar mnamo mwezi Desemba 2013.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger