Na
Bashir Yakub
Zipo namna nyingi
za kuachana kisheria
kwa wanandoa ambao
wanadhani sasa hawawezi kuendelea. Wengi wetu
tunajua zile za
kupitia mahakamani. Zile ni sahihi lakini
upo uwezekano pia wa
kuachana kwa mkataba
maalum bila kuhitaji
kwenda mahakamani.
Aidha yafaa ifahamike
kuwa Kuachana katika
ndoa na kuamua
kuishi nje ya
ndoa ni jambo
la kawaida. Kisheria si
dhambi mwanandoa yeyote
kuona kuwa sasa
hawezi kuendelea kuwa
katika ndoa. Ni
kwasababu hii hata
sheria ikatambua uwezekano
wa watu kuachana
na halikadhalika ikaweka
utaratibu maalum kwa
walio tayari kwa
hilo.
Tofauti na
kuachana kwa mkataba
namna nyingine ni
kwa njia ya
talaka mahakamani na kwa njia
ya kutengana mahakamani
ambazo nazo tutaziona hapa
chini kabla ya kutizama
ile ya mkataba.
1.KUACHANA KWA TALAKA.
Kifungu cha 99
cha Sheria ya
ndoa kinaongelea talaka.
Maombi ya talaka
hupelekwa na yule
anayedhani hawezi kuendelea
na ndoa kutokana
na sababu anazoamini
kuwa ndoa hiyo haiwezi kuendelea.
Mahakama huzisikiliza pande
zote mbili na
kuja na maamuzi.
Kifungu cha 107( 2 )
cha sheria ya
ndoa kinazitaja sababu
ambazo zote au
mojawapo ikithibitishwa ni
ushahidi kuwa ndoa
hiyo haiwezi kuendelea.
Baadhi ni ukatili, zinaa, kutelekeza, kifungo cha
maisha au kifungo
kisichopungua miaka mitano, na
nyingine nyingi.
Talaka huombwa mahakamani
na hivyo maombi yake hupelekwa mahakamani.
2. KUTENGANA MAHAKAMANI
BILA TALAKA.
Hatua hii ni
kwa mujibu wa kifungu
cha 99 cha
sheria ya ndoa.
Mnatengana kwa muda
fulani lakini bila
talaka. Talaka ni kutengana
milele wakati hii
ni kutengana kwa
muda. Njia hii
nayo muombaji hutakiwa
kwenda mahakamani na
kufungua maombi.
Wahusika wote wataitwa na kila mmoja atajieleza na baadae mahakama itatoa maamuzi. Njia hizi zote mbili mwombaji hutakiwa kupitia mahakamani isipokuwa hii ya mkataba ambayo itaelezwa hapa chini.
SHARE
No comments:
Post a Comment