Rais John Pombe Magufuli, akimpongeza
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul makonda, leo Machi 20, 2017 baada ya
kutoa hotuba ya ukaribisho kwenye hafla ya uwekaji jiwe la msingi
ujenzi wa Flyover Ubungo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Rais wa Benki
ya Dunia, Dkt. Jim Yong Kim.
NA
K-VIS BLOG
RAIS
John Pombe Magufuli, amemtetea Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na
kupuuza tuhuma mbalimbali zinazoendelea kutolewa dhidi ya Mkuu huyo wa Mkoa.
Akizunguzma
kwenye hafla ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara za juu kwenye
makutano ya barabara za Mandela, Morogoro na Sam Nujoma jijini Dar es Salaam
leo Machi 20, 2017, almaarufu kama Flyover, Rais Magufuli alisema. “Wana Dar es
Salaam tunatumia muda mwingi kwenye umbea, tunapoteza muda mwingi kujadili
personalities, niwaombe Wana-Dar es salaam tuache kupoteza muda tuchape
kazi, Mimi huwa sionyeshwi njia tayari
nimekwishaonyeshwa njia na chama change cha CCM kupitia Ilani ya uchaguzi,
swala la kuandikwa kwenye mitandao siyo tija kwangu.” Alisema.
Akifafanua
zaidi Rais Magufuli alsiema, yeye hatulazimishwa na mtu kufanya uamuzi Fulani kwani
anajiamini, “Makonda wewe chapa kazi, suala la kuandikwa kwenye mitandao si
tija kwangu wewe chapa kazi.” Alisisitiza Rais Magufuli.
Kauli
ya Rais Magufuli inakuja muda mfupi baada ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo, Nape Nanuye akiuunda kamati ya watu watano kuchunguza ni kwanini Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, “alivamia” studio za televisheni ya
Clouds akiwa na askari wenye bunduki usiku wa saa 4:45 Ijumaa iliyopita.
Akizungumza
wakati alipotembelea ofisi za Clouds Media Group, (CMG), huko Mikocheni B
jijini Dar es Salaam leo Machi 20, 2017, waziri Nape alisema, kamati
hiyo itafanya uchunguzi kwa masaa 24 na kuwasilisha ripoti kwake.
"Kitendo cha Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makodna, cha kuingia kwenye studio hizo
akiwa na
askari wenye silaha ni kuinajisi tasnia ya habari" Alisema Nape.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, anatuhumiwa kuingia kwa nguvu kwenye studio za Clouds
akiwa na askari wenye bunduki kwa nia ya kushinikiza ni kwanini habari ya mama
aliyefanyiwa mahojiano na watangazaji wa kipindi cha DE Weekend Chat Shaw,
(SHILAWADU), kuwa alizaa na Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Dkt. Josephat
Gwajima.
Hata
hivyo baada ya tathmini ya kitaalamu iliyofanywa ilionekana taarifa hiyo
isipeperushwe hewani kwani anayetuhumiwa hakupatikana ili nay eye aeleze upande
wake.
SHARE
No comments:
Post a Comment