Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Muhamasishaji
wa akaunti ya Malkia katika wiki ya wanwake Duniani kutoka benki ya
CRDB tawi la Water Front Mary Gekura amesema kuwa mpaka kufikia Machi 06
zaidi ya akaunti 100 za Malkia zimefunguliwa na zaidi wanawake wengi
bado wanaendelea kujitokeza kwa wingi.
Mary
amesema kuwa kuelekea katika kilele cha Wanawake Duniani bado
wanaendelea kuhamasisha wanawake wajitokeze kufungua akaunti hizo kwani
zina manufaa kwao na zinawapatia faida baada ya mwaka mmoja.
Akaunti
ya Malkia inamuwezesha mwanamke kuweza kupata mtaji au faida ya
kujiendeleza kiuchumi baada ya kuifungua na kuweka fedha kwa kipindi cha
mwaka mzima bila kutoa.
Muhamasishaji
wa akaunti ya Malkia katika wiki ya wanwake Duniani kutoka benki ya
CRDB tawi la Water Front Mary Gekura akimkabidhi fomu ya klufungulia
akaunti moja ya kina mama waliojitokeza kufungua akaunti hiyo kuelekea
kilele cha maadhimisho ya wiki ya wanawake Duniani Machi 08.
Muhamasishaji
wa akaunti ya Malkia katika wiki ya wanwake Duniani kutoka benki ya
CRDB tawi la Water Front Mary Gekura akimuelekeza namna ya kujaza fomu
ya kufungua akaunti ya wanawake ijulikanayo kama Malkia.
Wafanyakazi wa CRDB tawi la Water Front wakiwa katika picha za pamoja.
SHARE
No comments:
Post a Comment