Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Ole
Sendeka akizungumza na jumla ya wahitimu 90 wakati alipokuwa akifunga
jana mafunzo katika fani ya Utalii na Ukarimu yaliyoandaliwa na Wizara
ya Maliasili na Utalii na Mradi wa SPANEST yaliyofanyika Mkoani Njombe
kwa muda wa siku tatu. na Wengine ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Njombe, Joseph Choya (kulia) Mkurugenzi Msaidizi wa idara ya Utalii,
Paskasi Mwiru (kushoto)
Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Ole
Sendeka akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na
Maofisa kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Mradi wa SPANEST na
Halmashauri ya Wilaya ya Njombe mara baada ya kufunga mafunzo ya muda
wa siku tatu kwa jumla ya wahitimu 90 katika fani ya Utalii na
Ukarimu yaliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii na Mradi wa
SPANEST.
Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Ole
Sendeka akikabidhi cheti kwa Mhitimu wa mafunzo katika fani ya ukarimu
na utalii wakati alipokuwa akifunga mafunzo hayo jana yaliyoandaliwa na
Wizara ya Maliasili na Utalii na Mradi wa SPANEST yaliyofanyika Mkoani
Njombe.
Mkurugenzi Msaidizi wa idara ya
Utalii, Paskasi Mwiru alipokuwa akimkaribisha mgeni rasmi, Mkuu wa
mkoa wa Njombe kufunga mafunzo hayo katika fani ya Utalii na Ukarimu
yaliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii na SPANEST yaliyofanyika
jana Mkoani Njombe kwa muda wa siku tatu na yakiwa na jumla ya
washiriki 90.
Mkufunzi kutoka Chuo cha Taifa cha
Utalii (NCT), Dawson Kyungai akiwaelekeza Washiriki 90 wa Mafunzo ya
Ukarimu na Utalii namna ya kumimina mvinyo kwenye glasi pamoja na
kuwaonyesha kiwango kinachotakiwa. Mafunzo hayo yametolewa kwa muda wa
siku tatu katika fani ya mapokezi, utoaji huduma ya chakula na vinywaji
pamoja na upishi yaliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa
kushirikiana na Mradi wa SPANEST ambayo yamefungwa jana na Mkuu wa Mkoa
wa Njombe, Ole Sendeka .
Baadhi ya Wahitimu wa mafunzo
katika fani ya ukarimu na Utalii waliochaguliwa na wahitimu wenzao
mkoani Njombe ili kuunda chama chao cha wahudumu wa hoteli, migahawa na
nyumba za kulala wageni kitakachaowasaidia katika kurekebishana na
kupaza sauti zao katika utoaji huduma bora kwa watalii.
Mmoja kati ya Washiriki wa
mafunzo katika fani ya Ukarimu na Utalii akitoa nenpo la shukurani ya
mafunzo kwa Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na mradi wa
SPANEST kabla ya Mgeni rasmi kufunga jana mafunzo katika fani ya
ukarimu na Utalii.
Mratibu Msaidizi wa Mradi wa
SPANEST nchini, ( wa kwanza kushoto) akizungumza jinsi walivyojipanga
katika kuhakikisha Sekta ya utalii inakua kwa kasi kwa kuwapa mafunzo
wahudumu wa hoteli, nyumba za kulala wageni na migahawa katika fani ya
Utalii na Ukarimu yaliyoandaliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii na
SPANEST yaliyofanyika jana Mkoani Njombe kwa muda wa siku tatu.
…………………
Serikali kupitia Mkuu wa Mkoa wa
Njombe, Ole Sendeka amesema raia wa Kenya na Uganda wataendelea
kuajiriwa katika hoteli zetu kama Watanzania hawataweza kubadilika kwa
kuachana na tabia sizizofaa ambazo zimekuwa zikilalamikiwa na watalii
wengi wanaofikia katika hoteli hizo.
Amesema baadhi ya wafanyakazi
katika hoteli hizo wamekuwa na tabia za udokozi, uvivu na kiburi
akitolea mfano amesema unaweza ukafika katika hoteli ukakaa zaidi ya
nusu saa bila kusikilizwa huku wahudumu wakikupita tu kana kwamba
hawajakuona, hali inayochangia kwa watalii wanaotembelea vivutio vya
utalii kwa mara ya kwanza kutokurudi tena.
Akizungumza jana wakati akifunga
mafunzo yaliyofanyika kwa muda siku tatu mkoani Njombe kwa wahitimu 90
katika fani ya ukarimu na Utalii, alisema ni lazima wabadilike kwa
kufanya kazi kwa kujituma pasipo kusimamiwa na mameneja wa hoteli hizo
la sivyo wataendelea kulalamika huku nafasi zao zikiendelea kuchukuliwa
na wageni
Amesema wamiliki wengi wa hoteli
wamekuwa wakipenda kuajiri wafanyakazi kutoka nchi hizo kutokana na
uchapakazi wao na si kwa ajili ya wanajua lugha ya kiingereza
‘’Wamiliki wananchohitaji ni kupata faida na sio kung’ang’ania kuajiri
wazawa ambao hata kumkaribisha mgeni kwa bashasha imekuwa ni shida’’
alisisitiza Sendeka
Kufuatana na hali hiyo, amewataka
wahitimu wa mafunzo hayo katika maeneo ya mapokezi, utoaji huduma ya
chakula na vinywaji na upishi wakawe chachu katika kuchochea na
kuendeleza utalii nchini.
Naye, Mkurugenzi Msaidizi wa
Idara ya Utalii, Paskasi Mwiru amesema mafunzo hayo yanatarajiwa
kufanyika nchi nzima baada ya kugundua kuwa kuna idadi kubwa ya wafanya
kazi katika eneo hilo ambalo ni muhimu katika tasnia ya utalii ni watu
wenye ujuzi wa viwango vya chini na baadhi yao hawajapitia mafunzo
kabisa.
Alisema kumekuwa na vyuo vya
utalii vinavyoibuka kama uyoga na vimekuwa vikizalisha wahitimu wenye
ujuzi mdogo hali inayochangia kurudisha nyuma jitihada za serikali za
kuongeza idadi ya watalii wanotembelea vivutio vyetu vya utalii.
Kwa upande wa Mratibu Msaidizi wa
Mradi wa SPANEST, Edmund Murashani alisema mradi huo umeamua kujikita
katika kuwezesha wahudumu wa hoteli, migahawa na nyumba za kulala wageni
wanapata mafunzo kwa kuwa wao ni mojawapo ya nguzo muhimu katika
kuhakikisha utalii unakua katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.
‘’ Tunataka mtalii akifika katika
hoteli hizo kitu cha kwanza kabla hajatembelea vivutio vya utalii
vinavyopatikana katika ukanda huo awaze kuongeza siku za kulala katika
hoteli zetu kutokana na huduma stahiki anazopata kutoka kwa wahudumu
hao’’ Murashani alisema
Naye, Mhitimu wa Mafunzo hayo,
Tulizo Sanga aliomba siku za mafunzo hayo ziweze kuongezwa kwani siku
tatu hazitoshi kutokana na umuhimu wa mafunzo hayo kwao.
Mafunzo kama hayo yanatarajiwa
kufanyika mkoani Iringa na Songwe chini ya Usimamizi wa Wizara ya
Maliasili na Utalii kwa kushirikiana Shirika la Mpango wa Maendeleo la
Umoja wa Mataifa (UNDP) kupitia Mradi wa SPANEST unaotekelezwa na
Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA)
SHARE
No comments:
Post a Comment