Picha ya pamoja baina ya mkuu wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo wa nne kulia, akifuatiwa na diwani wa Vigwaza Mohsin Bharwani, na wa kwanza kulia ni Sukhwinder Jheetgh ambae ni mwenyekiti wa Khalsa Sports Club wafadhili wa Lions club dar es salaam-Panorama baada ya kambi ya siku mbili ya huduma ya macho Vigwaza. (picha na Mwamvua Mwinyi)
Mwenyekiti wa Khalsa
Sports Club, Sukhwinder Singh, akizungumza katika kambi ya huduma ya
macho iliyofanywa na Lions club dar es salaam -Panorama huko kata ya
Vigwaza kwa siku mbili. (picha na Mwamvua Mwinyi)
Mkuu wa mkoa wa Pwani
mhandisi Evarist Ndikilo, akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye
kambi ya huduma ya macho huko Vigwaza iliyofanywa na Lions club dar es
salaam -Panorama. (picha na Mwamvua Mwinyi)
Baadhi ya wakazi wa kata
ya Vigwaza,waliojitokeza kkwenye kambi ya huduma ya macho iliyofanywa
na Lions club dar es salaam -Panorama, wakisikiliza jambo katika kambi
hiyo. (picha na Mwamvua Mwinyi)
Diwani wa kata ya Vigwaza, Mohsin Bharwani akizungumza na baadhi ya wakazi waliojitokeza kwenye kambi ya macho iliyofanywa na Lions club dar es salaam -Panorama huko Vigwaza. (picha na Mwamvua Mwinyi)
Mkazi wa Vigwaza Sale
Juma akipimwa jicho katika kambi ya huduma ya macho iliyofanywa na Lions
club dar es salaam -Panorama huko shule ya msingi Vigwaza. (Picha na
Mwamvua Mwinyi).
…………….
Na Mwamvua Mwinyi, Vigwaza
WAKAZI zaidi ya 20 kata
ya Vigwaza, wilayani Bagamoyo,Pwani, wanatakiwa kufanyiwa upasuaji ili
kutibu ugonjwa wa mtoto wa jicho.
Aidha taasisi hiyo imetoa madaftari na vitabu vilivyogharimu sh.mil sita katika shule mbalimbali kwenye kata hiyo.
Akitoa taarifa katika
kambi ya macho iliyofanyika shule ya msingi Vigwaza ,mratibu wa taasisi
isiyo ya kiserikali ya lions dar es salaam -PANORAMA, Prash Bhatti,
alisema huduma ya macho waliyoitoa imegharimu mil. 30.
Alisema mbali ya kutoa huduma za macho ,pia waliwahudumia wagonjwa wa kisukari, presha na kusaidia huduma za kijamii.
Hata hivyo Bhatti
alisema kambi hiyo ilikuwa ni ya siku mbili ambapo watu 2,000
walijitokeza kupima macho na kupata huduma ya miwani bure .
“Shida kubwa ni ugonjwa
wa mtoto wa jicho ambao kitaalamu tunaita cataract ugonjwa huu ndio
unaoongoza kwa kuharibu jicho, dawa yake ni upasuaji”alisema.
Bhatti alielezea,watu hao waliogundulika na mtoto wa jicho watafanyiwa upasuaji na gharama zote zitatolewa na lions club.
Alisema tatizo hilo la
mtoto wa jicho lisipopata matibabu mapema husababisha upofu na
kusababisha mtu kuishi katika hali y’all umaskini.
Nae mkuu wa mkoa wa
Pwani mhandisi Evarist Ndikilo,alitoa wito kwa jamii kupima macho mara
kwa mara ili tatizo libainike mapema na kutibiwa.
Aliiasa jamiii kufanya matibabu ya mtoto wa jicho hospitali badala ya kukaa majumbani bila kujitibia.
Mhandisi Ndikilo,
alisema tiba ya ugonjwa huo ni upasuaji na kuwa ulaji mzuri wa chakula
na matunda hukinga macho dhidi ya magonjwa mbalimbali.
“Nampongeza diwani wa
kata hii Mohsin Bharwani kwa kuona umuhimu wa kuwatumikia wananchi wake
ikiwemo masuala ya kiafya”alisema mhandisi Ndikilo.
Diwani wa kata ya
Vigwaza, Mohsin Bharwani aliishukuru taasisi hiyo kwa kujitolea kutoa
huduma mbalimbali za afya na vitabu mashuleni.
Alifafanua kwamba watu wengi huwa hawapendi kuchunguza afya zao hivyo lions club imekuwa mkombozi kwao.
Bharwani, alishukuru pia kupokea msaada wa vitabu na madaftari kwa wanafunzi wa shule zilizopo Vigwaza.
SHARE
No comments:
Post a Comment