Mwalimu
wa somo la Baiolojia katika shule ya sekondari ya wasichana ya St
Therese ambaye alidakwa akifanya mapenzi na mwanafunzi katika maabara
ya shule hiyo amesimamishwa kazi akisubiri hatua za kinidhamu dhidi
yake.
Ofisa
Elimu wa Wilaya, Christopher Sinkamba akizungumza alisema kwamba
maamuzi hayo yamechukuliwa baada ya wananchi wengi kulalamika.
Sinkamba alisema mwalimu anayehusika ametambuliwa kama Raphael Mwape na kwamba sasa anasubiri hatua za kinidhamu dhidi yake.
Alisema
kwamba utawala wa shule ulifikisha suala hilo Polisi lakini walishindwa
kumshtaki kwa tuhuma za kubaka kwa kuwa binti huyo ni zaidi ya miaka
16.
Na
wakati alipoulizwa swali kwanini mwanafunzi huyo wa kike ametimuliwa
shule, ofisa huyo alisema kwamba hawajamfukuza lakini walilazimika
kumhamisha shule kutokana na sheria za shule hiyo.
Ilielezwa
kuwa tukio hilo lilifanyika saa 12 jioni ambapo Mwape alionwa na
mabinti wengine wawili wa shule hiyo akifanya mapenzi na binti huyo
katika maabara B ya shule hiyo.
Mwanafunzi
huyo alisema kwamba hiyo haikuwa mara ya kwanza kwa mwalimu huyo
kumuingilia na kwamba siku hiyo alilazimika kufanya hivyo baada ya
kushinikizwa na mwalimu aliyemuita wakati akirejea bwenini.
Alisema pamoja na kukataa kwake alimshinikiza kwa kudai kuwa alikuwa amemgharamia sana. Mwalimu huyo ana mke.
SHARE
No comments:
Post a Comment