Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Susan Kolimba (katikati),
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya ziara ya
siku mbili ya kitaifa ya Waziri Mkuu wa Ethiopia, Mhe. Hailemariam
Dessalegn nchini. Waziri Mkuu huyo atawasili nchini tarehe 31 Machi,
2017 asubuhi na kupokelewa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. Akiwa nchini atakutana kwa
mazungumzo na Mhe. Rais Magufuli pamoja na kutembelea Bandarini.
Wengine katika picha ni Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Mhe. Balozi
Naimi Aziz (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika, Balozi
Innocent Shiyo (kulia).
SHARE
No comments:
Post a Comment