Uongozi wa klabu ya Yanga ya jijini Dar
es salaam,umesema kwamba kwa sasa nguvu zao wanazielekeza kwenye michezo
yao ya ligi kuu ya Tanzania bara iliyosalia ukiwemo mchezo wao dhidi ya
Azam FC utakaopigwa siku ya tarehe moja ya mwezi wa nne mwaka huu.
Katibu mkuu wa Yanga Charse Boniphace Mkwasa,amesema kuwa baada ya
kuondoshwa kwenye michuano ya klabu bingwa barani Afrika dhdi ya Zanaco
kwa sasa nguvu zao zote zinaelekezwa kwenye ligi.
Mkwasa amesema kwamba kwa sasa wanasubiri lipoti ya kocha mkuu kufahamu
progarm zake za mazoezi hii inatokana na timu hiyo kurejea hapo jana
wakitokea nchini Zambia walipokwenda kushiriki mchezo wa kimtaifa dhidi
ya Zanaco.
Alisema kwamba hata ratiba ya ushiriki wao kwenye shirikisho
walipoangukia wanategemea kupata taarifa lipoti hiyo ya kocha George
Lwandamina kuhusu mipango yake.
No comments:
Post a Comment