Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameonya kuwa Libya
ipo katika hatari ya kurejea katika mgogoro wa nchi nzima, akidokeza
kuhusu hali tete ya usalama mjini Tripoli na mapigano yanayoendelea
katika maeneo ya mashariki yenye hazina ya mafuta na maeneo mengine.
Antonio Guterres
Ametoa tahadhari hiyo katika ripoti aliyoitoa kwa Baraza la Usalama la
Umoja wa Mataifa kutokana na kuanza tena ongezeko la mapambano ya
kijeshi pamoja na mkwamo wa kisiasa katika taifa hilo.
Aidha Guterres
amesema wapiganaji wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu, kwa hivi sasa
halina tena udhibiti nchini Libya, lakini athari zake zimeendelea
kushuhudiwa, limekuwa likihusishwa na mashambulizi kadhaa katika maeneo
tofauti, na jumuiya ya kimataifa katika taifa hilo bado ni shabaha ya
mashambulizi.
Kuondoshwa kwa mtawala wa muda mrefu wa Libya Muammar
Gaddafi mwaka 2011 kumeiingiza Libya katika machafuko.
No comments:
Post a Comment