TRA

TRA

Saturday, April 15, 2017

Wadukuzi wametoa nyaraka na mafaili ya NSA kuchunguza miamala ya mabenki

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


Wadukuzi wametoa nyaraka na mafaili ambayo wataalamu katika masula ya usalama mitandani wanasema inaonesha kuwa Shirika la Usalama wa taifa la Marekani limeweza kuingilia mfumo wa utambuzi wa mawasiliano ya miamala kupitia benki , SWIFT, jambo linalotoa uwezo wa kufuatilia mwenendo wa kifedha katika mabenki katika baadhi ya mataifa ya Mashariki ya Kati na Kusini mwa Amerika. 


            Rais Donald Trump
Mshauri wa masula ya usalama mitandaoni Shane Shook amesema taarifa hiyo inajumuisha namba za siri za kompyuta ambazo zinaweza kutumiwa na wahalifu kuingia katika eneo la uhifadhi wa kumbukumba na kuangalia mwenendo wa taarifa.

Nyaraka hizo na mafaili zilitolewa na kundi linalojiita madalali kivuli. Baadhi ya rekodi zina alama za NSA , lakini shirika la habari la Reuters halikuweza kuthibitisha uhalisia wake.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger