Jengo jipya la CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja Kichama
lililopo katika kijiji cha Mahonda Wilaya ya Kaskazini “B” Unguja.
NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt. Abdalla Juma
Saadalla “Mabodi” amewaagiza Watendaji na Viongozi wa Chama na
Jumuiya zake kuwa wabunifu kwa kuanzisha miradi ya kudumu ya kimaendeleo.
Agizo hilo amelitoa katika ziara yake huko Mkoa wa
Kaskazini Unguja alipotembelea jengo jipya la kisasa la ofisi ya Mkoa
huo, huko Mahonda Unguja, alisema jengo hilo limekamilika kwa muda mwafaka
ambao Chama hicho kipo katika mkakati maalum wa kuwa na vitega uchumi imara
vitavyosaidia chama kujitegemea katika masuala ya kiuchumi.
Dkt. Mabodi alieleza kwamba Chama hicho kwa Zanzibar
lazima kila ngazi ya kiutendaji kuanzia katika Mashina hadi Taifa ni lazima
wawe na miradi ya maendeleo kupitia rasilimali ardhi na baadhi ya majengo
waliyokuwa nayo ili waweze kujipatia kipato kitakachosaidia kutatua changamoto
za ukata wa fedha hasa katika masuala ya kiutendaji na kijamii.
Aliwambia wanachama CCM Zanzibar kwamba nia ya muundo
na marekebisho ya Katiba ya Chama ni kuhakikisha utamaduni wa chama kutegemea
ruzuku za serikali sambamba na ngazi zote za chama na jumuiya kuona zinaanza
mapema kujiandaa kisaikolojia kwa kuanzisha miradi na vitega uchumi.
“ Kwanza nakupongezeni kwa juhudi zenu za kujenga
jengo la kisasa la ofisi linaloendana na hadhi ya CCM, lakini kubwa ni kwamba
ndani ya jengo hili mmeweka vitega uchumi vya kuzalisha mapato yatakayosaidia
katika shughuli za uendeshaji.
Rai yangu kwenu na Mikoa mingine ya Kichama pamoja na
Jumuiya zake, tuanze rasmi kuenzi busara za Waasisi wetu ambao ni Marehemu
Abeid Amaan Karume na wenzake ili serikali na chama tawala vijitawale kiuchumi
na kimaendeleo.”, alisema Dkt. Mabodi.
Akizungumza Mwenyekiti wa
CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja, Haji Juma Haji alisema jengo hilo limejengwa kwa
juhudi za ungozi wa Mkoa huo kwa kushirikiana na wanachama wengine waliokubali
mwekezaji ajenge jengo hilo ili wapate fursa mbali mbali za kiuchumi.
Bw. Haji pia aliweka wazi kwamba licha
ya kuwepo na vikwazo vya majukungu na kauli zisizofaa kutoka kwa baadhi ya
wapinga maendeleo, lakini wameweza kulikamilisha na kwa sasa kilichobaki ni
kuwekwa vifaa vya samani ili liweze kuzinduliwa rasmi.
Akitoa ufafanuzi juu ya jengo hilo, Katibu wa CCM Mkoa
huo, Bw. Mulla Othman Zubeir amesema jengo hilo limeanza kujengwa
toka mwaka 1986 na baadae liaachwa lakini uongozi wa mkoa huo wa sasa
uliamua kuliendeleza kwa msaada wa Mwekezaji ambaye ni Bw. Braiyan
Somson kupitia mradi wake wa Pen Royal ameweza kujenga jengo hilo bila
masharti yoyote.
Katibu Bw. Mulla alieleza kwamba Mwekezaji huyo
amekuwa ni miongoni mwa watu muhimu waliosaidia kufanikisha ofisi hiyo ya
kisasa kwani ameonyesha mapenzi na nia ya kweli ya kukiunga mkono chama cha
Mapinduzi
Ofisi hiyo imejengwa kwa gharama zinazokadiriwa
kufikia zaidi ya shilingi milioni 300 pia ina vitengo vyote Chama na
Jumuiya zote kwa ngazi mbali mbali za Mkoa huo pamoja na vyumba vya ukodisha
maduka ili mkoa huo upate fedha za kuongeza kipato katika shughuli za
kiutendaji.
Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa huo Bw. Haji Juma Haji
akitoa ufafanuzi juu ya mambo mbali mbali yanayohusu jengo hilo mbele ya
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdalla Juma Saadalla “Mabodi”
alipokuwa katika ziara yake ya kuimarisha chama ndani ya Mkoa huo.
SHARE
No comments:
Post a Comment