Suala la Syria linatarajiwa kuwa juu katika mkutano wa leo wa mawaziri wa mambo ya kigeni wa kundi la mataifa yaliyoendelea kiviwanda G7, wakati waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Rex Tillerson akiangaziwa zaidi kabla ya kuelekea Moscow , mshirika mkuu wa rais Bashar al-Assad.
Mawaziri hao wa mambo ya kigeni wanatarajiwa kutoa wito wa msukumo mpya kumaliza vita nchini Syria.
Lakini mawaziri hao wanatofautiana juu ya vipi kuweka mbinyo dhidi ya Urusi kuhusiana na hatua yake ya kumuunga mkono rais Bashar al-Assad, ambae majeshi yake yanalaumiwa kwa shambulio baya la gesi ya sumu wiki iliyopita.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Sigmar Gabriel amesema Urusi na Iran , zinapaswa kuhusishwa katika hatua za amani , na msemaji wa waziri wa mambo ya kigeni wa Japan Masato Ohtaka amesema Urusi inaweza kuchukua jukumu muhimu katika hatua hizo.
Lakini waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza Boris Johnson amechukua msimamo mkali zaidi, akisema vikwazo vipya vinatarajiwa ili kuisukuma Urusi kusitisha hatua yake ya kumuunga mkono Assad.
SHARE
No comments:
Post a Comment