Marekani imefanya hitimisho la awali kwamba Urusi ilifahamu mapema kuhusu shambulio la gesi ya sumu wiki iliopita, lakini haina ushahidi kuhusu ushiriki wa Moscow katika shambulizi hilo.
Afisa mwandamizi wa serikali ya Marekani amesema ndege isiyo rubani inayoendeshwa na Warusi ilikuwa ikiruka juu ya hospitali wakati waathirika wa shambulizi hilo wakikimbia kupata matibabu.
Rais Vladmir Putin
Saa chache baada ya ndege hiyo kuondoka, ndege ya kivita iliotengenezwa nchini Urusi ilishambulia hospitali hiyo, katika kile ambacho maafisa wa Marekani wanaamini lilikuwa jaribio la kuficha utumiaji wa silaha za kemikali.
Afisa huyo wa Marekani amesema uwepo wa ndege ya uchunguzi isiyo na rubani juu ya hospitali hiyo hakuwezi kuwa jambo lisilokusudiwa, na kwamba Urusi lazima ilijua kuwa shambulizi la kemikali lilikuwa linakuja na kwamba waathirika walikuwa wanatafuta matibabu.
SHARE
No comments:
Post a Comment