KAMISHINA wa Operesheni na Mafunzo wa jeshi la polisi,
Nsato Marijani, akizungumza na waandishi wa habari kwenye Ofisi za
Wizara ya Mambo ya Ndani, wakati akitoa tamko kuhusu operesheni
itakayoendeshwa na jeshi hilo ya kuwasaka wahalifu waliohusika na mauaji
ya Askari nane katika msitu wa Jaribu Mpakani Mkoa wa Pwani juzi.
Kushoto ni Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Bulimba ''Tunaomba
wananchi watusamehe kwa operesheni hii tunayokwenda kuianza, kwani
askari wanane ni wengi sana na hatutakuwa na msalie mtume kwa hili,
wameanza sisi tunamaliza, na jana ilikuwa ni 8 - 4, lakini tukianza
nawaambia mabao yetu yatakuwa ni zaidi yao'';. alisema Marijani Aidha
Marijani ametangaza kuwa eneo hilo ni marufuku waendesha pikipiki kupita
zaidi ya saa kumi na moja jioni. Kaa nasi (KWA HISANI YA SUFIANI MAFOTO BLOG)
SHARE
No comments:
Post a Comment