TRA

TRA

Saturday, April 15, 2017

Tulaani sote tukio la Polisi kuuawa - Godbless Lema

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !



Tukio la kuuawa askari wa Jeshi la Polisi linapaswa kulaaniwa kwa nguvu zote na kila Raia wa Taifa letu , hii ni dalili mbaya sana kwa ustawi wa amani ya Taifa letu . Hata hivyo ninamuomba Mungu awatie nguvu , ndugu , rafiki na familia zote za marehemu waliofikwa na msiba huu mbaya sana na mzito .

Polisi wameuwawa wakiwa kwenye wajibu wao wa kulinda raia na mali zao ni muhimu sasa kwa vyombo vya usalama kuwatia nguvuni na kuthibiti kwa weledi matendo kama haya yanayoendelea kushamiri kwa kasi sana , ni muhimu pia idara za ulinzi na usalama kufanya utafiti wa kina kujua ni nini haswa sababu za matukio kama haya.

Hatuwezi kuishi kwa amani bila ya kuwa na Jeshi la Polisi imara na ili tuwe na Jeshi la Polisi imara , tunapsawa kuwa na jamii inayotoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi haswa kwenye nyakati ngumu kama hizi , hivyo ni matumaini yangu kuwa Wananchi wote hususani wa maeneo hayo yalipotokea mauaji watakuwa tiyari kutoa ushirikiano ili kuwabaini wahusika wa tukio hili baya.


 Godbless Lema ( MB)
Waziri Kivuli Mambo ya Ndani.






Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger