Na Jimmy Mengele - Dodoma.
Mfuko
wa Pensheni wa PPF unaendelea kuwakumbusha wananchi kujiunga na PPF ili
kuweza kufaidika na fursa mbalimbali kama vile mikopo ya maendeleo,
elimu, huduma ya afya, mafao ya uzeeni na mafao ya uzazi.
Akiongea
katika Maonesho ya uwezeshaji wananchi kiuchumi katika viwanja vya
Mashujaa, mkoani Dodoma, Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PPF Janet Ezekiel
alisema hii ni fursa pekee kwa waajiriwa wapya wakiwemo walimu,
madaktari na kada zingine kuchagua Mfuko wa Pesheni wa PPF ili kuweza
kukidhi mahitaji yao ya kimaendeleo.
Afisa
huyo alisema waajiriwa hao wapya wakijiunga na PPF watafaidika na
mikopo katika maeneo yao ya kazi, mafao ya uzazi, mafao elimu, mafao ya
ugonjwa, mafao ya kifo, wategemezi, kiinua mgongo na mafao ya uzeeni
yanayolipwa kwa wakati kwa kutumia kikotoo kilichoboreshwa.
Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Anthony Peter Mavunde
akisaini kitabu cha wageni katika banda la PPF katika Maonesho ya Mifuko
ya uwezeshaji wananchi kiuchumi baada ya kupata maelezo ya mpango wa ‘
Wote scheme’ ambao umekua msaada katika kuwaongezea mitaji vijana
kutokana na mikopo ya mpango huo, waliosimama Afisa Uhusiano Mwandamizi
wa PPF Janet Ezekiel na Afisa Mfawidhi wa PPF Astro Liganga.
Afisa
Uhusiano Mwandamizi wa PPF Janet Ezekiel na Afisa Mfawidhi wa PPF Astro
Liganga wakitoa maelezo juu ya huduma za PPF kwa Waziri wa
viwanda,biashara na uwekezaji Mhe. Charles Mwijage wakati alipotembelea
Maonesho ya Mifuko ya uwekezaji kiuchumi katika viwanja vya Mashujaa
mkoni Dodoma.
Afisa
Mwendeshaji wa PPF, Kanda ya Mashariki na Kati Joyce Rwechungura akitoa
maelezo ya kazi mbalimbali zinazofanywa na PPF kwa waliotembelea banda
la PPF katika Maonesho ya Mifuko ya uwezeshaji wananchi kiuchumi
inayoendelea katika viwanja vya Mashujaa mkoni Dodoma.
Mbunge
wa jimbo la Kishetu, Elias Kwandikwa akiuliza swali juu mpango wa
‘Wote scheme’ ulivyofanikiwa kwa watu wote ikiwemo walio kwenye Sekta
isiyo rasmi nao kupata nafasi ya kupata mafao mbalimbali. Wanaomfuatilia
kwa makini ni Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PPF Janet Ezekiel na Afisa
Mfawidhi wa PPF Astro Liganga.
Katibu
wa Chama cha Wafugaji Tanzania Magembe Makoye akimsikiliza kwa makini
Afisa Mfawidhi wa PPF Astro Liganga kuhusu Mfumo wa ‘Wote scheme’ ambao
kima cha chini cha kuchangia ni shilingi elfu ishirini na ndani yake
kuna fursa za mikopo ya maendeleo, mikopo ya elimu, huduma za afya na
mafao ya uzeeni. Mfumo huu unawawezesha wote walio katika sekta isiyo
rasmi kujiwekea akiba.
Michael
Silasi (mwenye miwani ) na Said Ally (aliyevaa kofia ) wakimsikiliza
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PPF Janet Ezekiel kuhusu kazi za PPF na
mafao yanayotolewa na Mfuko huo ikiwemo mfumo wa 'Wote scheme' ambao
utoa fursa za mikopo ya maendeleo, mikopo ya elimu, huduma za afya na
mafao ya uzeeni. Mfumo huu unawawezesha wote walio katika sekta isiyo
rasmi kujiwekea akiba.
SHARE
No comments:
Post a Comment