Rais Magufuli
Rais
Magufuli amesema kumekuwa na changamoto kubwa katika kila sekta hivyo
sasa anasubiri hiyo ripoti ili aweze kuifanyika kazi na kutenda haki
katika jambo hilo.
"Naisubiri ripoti ya wafanyakazi wa Serikali zaidi ya elfu tisa ambao wana vyeti vya kufoji ili niifanyie kazi" alisema Rais Magufuli
Mbali na hilo Rais Magufuli ameitaka Taasisi ya TCU kuacha kuwapangia
wanafunzi vyuo bali wanafunzi wanapaswa kuwa huru kuchagua aina ya vyuo
ambavyo wao wanataka kwenda na kusema kwa kufanya hivyo itatoa nafasi
kila chuo kuwa na wanafunzi wa kutosha huku wanafunzi pia wakienda
kusoma sehemu ambazo wao wanahitaji kwenda kusoma na si kuwapangia.
"Mtu amefaulu ana sifa zake
anataka kuja kusoma Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam afaidi mabweni ya
Magufuli analazimishwa kupelekwa kwenye ka chuo ambako wala hakana jina
hata ukitafuta kwenye mtandao hakaonekani, akasome pale wakati hawana
hata mabweni na saa zingine hata walimu hawana, tunawatesa watoto hawa
na saa zingine wakuu wa vyo vile wamekuwa na tabia ya kwenda kwenye
uongozi wa TCU ingawa sina ushahidi wapangiwe idadi wa wanafunzi
wanaowataka kwenye vyo hivyo, sifahamu wanapangiwa kwa rushwa lakini
wapo pia kuna ushahidi na baadhi ya viongozi wa vyuo fulani fulani
waliofunga safari kwenda TCU kwa ajili ya kuomba wapangiwe wanafunzi au
kutoa shukrani, au hata kwenda kuwasalimu tu" alisema Rais Magufuli
SHARE
No comments:
Post a Comment