Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Syria, Iran na Urusi wameionya Marekani
dhidi ya mashambulizi yake kwa Syria katika mkutano wao uliofanyika
mjini Moscow Urusi.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergey Lavrov,
pamoja na wenzake wa Iran na Syria wamelishitumu vikali shambulizi la
anga la hivi karibuni lililofanywa na Marekani katika kambi ya kikosi
cha anga cha Syria.
Bashar Assad
Lavrov amesema hatua yoyote nyingine kama hiyo
itakayochukuliwa na Marekani itakuwa na athari kubwa kwa usalama wa
dunia.
Hata hivyo wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema taifa hilo
halijafanya uamuzi wowote mwingine wa kufanya mashambulizi zaidi.
Msemaji wa wizara hiyo Mark Toner amesema Urusi ingetumia ushawishi wake
kwa Assad kuhakikisha vita katika taifa hilo la Mashariki ya Kati
vinamalizika kabisa.
No comments:
Post a Comment