Maelfu ya waumini wa madhehebu ya Kikatoliki walikusanyika katika
uwanja wa kanisa kuu mjini Vatican kwa lengo la kufanya maandamano ya
kumbukumbu ya kifo cha Yesu Kristo.
Papa Francis ambae awali alishiriki
katika ibada ya Ijumaa Kuu katika kanisa la mtakatifu Peter , Basilika,
alihudhuria na kusali kwa dakika kadhaa katika madhabahu.
Katika
maandamano alishika msalaba huku akisindikizwa na waumini wengine
waliokuwa na mishumaa.
Maandamano haya ya mwaka huu yamefanyika katika
ulinzi mkali baada ya kutokea mashambulizi ya lori katika miji kama
Berlin, London na Stockholm.
SHARE
No comments:
Post a Comment