Aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu amewataka
wananchi kumpa ushirikiano IGP mpya, Simon Sirro katika kukabiliana na
matukio ya uhalifu nchini hasa katika Mkoa wa Pwani.
Mangu ameyasema hayo leo Ikulu jijini Dar es salaam baada ya Rais John
Magufuli kumwapisha Sirro kuongoza jeshi la polisi nchini.
Mangu ambaye anasubiri kupangiwa kazi nyingine amesema anamfahamu Sirro
kama mchapakazi mzuri na ataweza kutekeleza majukumu yake ya kuhakikisha
kwamba Tanzania inakuwa na amani.
Alipoulizwa wito wake kwa Sirro kuhusiana na hali tete katika wilaya za
Rufiji na Kibiti mkoani Pwani, Mangu amesema "Sirro anafahamu
anachotakiwa kufanya katika hilo, nimefanya naye kazi kwa karibu,
ninachoomba ni askari na wananchi wote wampe ushirikiano."
Sirro ameapishwa leo kuwa IGP, kabla ya uteuzi huo alikuwa kamanda wa
polisi (RPC) katika mikoa ya Tanga, Mwanza na Shinyanga. Baadaye
alikwenda kitengo cha operesheni na mafunzo polisi makao makuu, kisha
akahamishiwa kitengo hicho kanda maalumu ya Dar es Salaam kabla ya kuwa
kamishna wa kanda hiyo.
SHARE
No comments:
Post a Comment