TRA

TRA

Friday, May 26, 2017

Bei ya mafuta yashuka kwa 5% duniani

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


Bei ya mafuta imeshuka kwa asilimia 5 licha ya mataifa yanayozalisha bidhaa hiyo kukubaliana kupunguza kiwango cha uzalishaji kwa kipindi cha miezi minane.

Wakikutana mjini Vienna,mawaziri wa kawi kutoka muungano wa mataifa yanayozalisha mafuta OPEC na mataifa yasiozalisha bidhaa hiyo ulikubaliana kuendelea kupunguza kiwango cha mafuta hadi Machi 2018.
Lakini wawekezaji walikuwa na matumani kwamba wazalishaji hao wa mafuta wataendelea na mpango huo.

Mafuta ghafi yalishuka kwa dola 2.60 hadi dola 51.36 kwa pipa siku ya Alhamisi na yalikuwa yamefika dola 51.47 Ijumaa alfajiri. 

Waziri wa kawi nchini Saudia Khalid al-Falih aliyesimamia mkutano huo kama mwenyekiti mwenza na mwenzake wa Urusi Alexander Novak alisema: Tuliangazia vigezo kadhaa kutoka miezi 6, 9 na hadi 12 na pia tuliangazia uwezekano wa kupunguza uzalishaji huo kwa viwango vya juu.

Muungano wa mataifa ya OPEC na mataifa mengine 11 yasiozalisha mafuta ikiwemo Urusi, kwanza yalikubaliana kupugunza uzalishaji Disemba iliopita katika juhudi za kupiga jeki bei.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger