Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa
Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), Bw. Francis Assenga (kushoto) akizungumza
na Katibu Tawala Mkoa wa Mkoa wa Arusha, Bw. Richard Kwitega (hayupo pichani)
wakati walipomtembelea Ofisini kwake kuzungumzia fursa za uwekezaji mkoani
Arusha. Kulia ni Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB, Bw. Augustino
Chacha.
Katibu Tawala Mkoa wa Mkoa wa
Arusha, Bw. Richard Kwitega (katikati) akizungumza na ugeni kutoka TADB wakati
walipomtembelea Ofisini kwake kuzungumzia fursa za uwekezaji mkoani Arusha.
Ugeni uliongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga.
Katibu Tawala Mkoa wa Mkoa wa
Arusha, Bw. Richard Kwitega (katikati) akizungumza na ugeni kutoka TADB wakati
walipomtembelea Ofisini kwake kuzungumzia fursa za uwekezaji mkoani Arusha.
Ugeni uliongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga.
Katibu Tawala Mkoa wa Mkoa wa
Arusha, Bw. Richard Kwitega akihimiza jambo wakati alipokuwa akizungumza na
ugeni kutoka TADB wakati walipomtembelea Ofisini kwake kuzungumzia fursa za
uwekezaji mkoani Arusha.
Mkurugenzi wa Mikopo na
Biashara wa TADB, Bw. Augustino Chacha (kulia) akizungumzia fursa za mikopo
inayotolewa na Benki wakati akizungumza na Katibu Tawala Mkoa wa Mkoa wa
Arusha, Bw. Richard Kwitega (hayupo pichani). Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), Bw. Francis Assenga.
Meneja wa Uendelezaji wa
Biashara wa TADB, Bw. Geofrey Mtawa (kulia) akitoa takwimu za mahitaji ya
mikopo ya mkoa wa Arusha. Kushoto ni Afisa Mwandamizi wa Uendelezaji wa
Biashara wa TADB, Bw. George Nyamrunda.
Katibu Tawala Mkoa wa Mkoa wa
Arusha, Bw. Richard Kwitega (kushoto) akimkabidhi muhtasari wa maeneo ya
uwekezaji Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), Bw.
Francis Assenga (kulia).
NA MWANDISHI WETU
Wito umetolewa kwa Benki
ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB) kuchangamkia fursa za uwekezaji
katika serkta ya kilimo na mifugo kwa kuwapatia mikopo wakulima
wanaojishughulisha katika sekta hizo mkoani Arusha ili kuchagiza sekta ya
kilimo mkoani humo.
Wito huo umetolewa na Katibu
Tawala Mkoa wa Mkoa wa Arusha, Bw. Richard Kwitega wakati akizungumza na ugeni
kutoka TADB wakati walipomtembelea Ofisini kwake kuzungumzia fursa za uwekezaji
mkoani Arusha.
Bw. Kwitega amesema kuwa mkoa
wa Arusha una fursa nyingi za uwekezaji hasa katika maeneo ya kilimo na
ufugaji.
Akizungumza wakati wa
mazungumzo hayo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Bw. Francis Assenga
alisema uanzishwaji wa TADB unatokana na Serikali kutambua umuhimu wa uwekezaji
wenye tija kwenye maeneo yote ya sekta ya Kilimo na kuleta mapinduzi ya dhati
ya Kilimo ili kuwezesha upatikanaji wa mikopo na mitaji ya riba nafuu ikiwa
ni pamoja na kuhamasisha mabenki na taasisi zingine za fedha nchini kutoa
mikopo zaidi kwenye sekta ya Kilimo.
Bw. Assenga mkoa wa Arusha
utaingizwa rasmi katika mpango wa biashara wa Benki na ametoa wito kwa wakulima
na wafugaji wa mkoa wa Arusha kuchangamkia fursa zinazotolewa na TADB.
SHARE
No comments:
Post a Comment