Rais wa Marekani
Donald Trump amesisitiza kwamba hafanyiwi uchunguzi wowote baada ya
kumfuta kazi mkurugenzi wa shirika la ujasusi la FBI.
Bwana Trump aliambia chombo cha habari cha NBC kwamba ilikuwa uamuzi wake pekee kumsimamisha kazi James Comey.Bwana Comey alikuwa akiongoza uchunguzi kuhusu madai ya Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani uliokamilika mbali na uwezekano kwamba kulikuwa na mawasiliano kati ya, maafisa wa Trump na Urusi wakati wa kampeni.
Bwana Trump ameutaja uchunguzi huo kuwa unafiki mkubwa madai yaliopingwa na Mrithi wa Comey.
- Mfasiri wa FBI afunga ndoa na mwajiri wa IS
- Clinton: Nalaumu FBI na wadukuzi wa Urusi
- Mkurugenzi wa FBI apinga madai ya Trump kuhusu Obama
Nilimwambia iwapo inawezekana unaweza kuniambia, Je Ninachunguzwa? Aliniambia ,huchunguzwi.
''Najua sichunguzwi'', Bwana Trump alimwamabia aliyekuwa akimhoji, akirejelea madai aliyotoa katika baraua ya Jumanne ya kumfuta kazi bwana Comey.
Rais huyo pia alipinga maelelezo ya ikuu ya Whitehouse kwamba alimfuta bwana Comey baada mapendekezo kutoka maafisa wakuu wa wizara ya haki.
SHARE
No comments:
Post a Comment