Ofisa
Mkuu wa Wateja Wakubwa na Serikali wa Benki ya NMB, Richard Makungwa
(kulia), akimkabidhi Katibu wa Timu ya Singida United, Abdurahman Sima,
mipira na vifaa vingine vya michezo vyenye thamani ya sh,milioni 10 Dar
es Salaam jana kwa ajili ya maandalizi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania
Bara itakayoanza Agosti mwaka huu.
Katibu wa Timu ya Singida United, Abdurahman Sima (kushoto), akizungumza wakati wa hafla fupi ya kupokea vifaa hivyo.Ofisa Mkuu wa Wateja Wakubwa na Serikali wa Benki ya NMB, Richard Makungwa (katikati), akizungumza katika hafla ya kukabidhi vifaa hivyo. Kulia ni Mwenyekiti wa timu hiyo, Yusuph Mwandani.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Hapa ni makabidhiano ya jezi.
Vifaa vilivyokabidhiwa vikioneshwa kwa wanahabari.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Ofisa Mkuu wa
Wateja Wakubwa na Serikali wa Benki ya NMB, Richard Makungwa (katikati),
akisisitiza jambo baada ya kukabidhi msaada huo.
Na Dotto Mwaibale
BENKI ya
NMB imetoa msaada wa vifaa vya michezo vyenye thamani ya sh. milioni 10
kwa timu ya Singida United kwa ajili ya maandalizi ya Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania Bara itakayoendelea kuanzia mwezi Agosti mwaka huu.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi msaada huo makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es
Salaam jana, Ofisa Mkuu wa Wateja Wakubwa na Serikali, Richard Makungwa
alisema msaada huo umelenga kusaidia timu hiyo kwa ajili ya kujiandaa
kwa ligi hiyo.
“Tumetoa
msaada huu kwa timu ya Singida United kwa kwa ajili ya maandalizi ya
ligi hiyo na hii ni kawaida yetu kusaidia timu mbalimbali pale
tunapopata nafasi” alisema Makungwa.
Makungwa
alisema licha ya benki hiyo kufanya shughuli za kibenki pia imejikita
kuinua michezo nchini kwa kutoa msaada wa vifaa vya michezo.
Alitaja
vifaa walivyotoa msaada kwa timu hiyo ni viatu vya mpira wa miguu, jezi
na mipira vyote vikiwa na thamani ya sh.milioni 10.
Katibu wa timu hiyo Abdurahman Sima alisema vifaa hivyo walivyopata vitatumika kwa lengo lililokusudiwa na si vinginevyo.
“Tunaishukuru benki ya NMB kwa msaada huu tunaomba wadau wengine kuiga mfano wa benki hii ” alisema Sima.
SHARE
No comments:
Post a Comment