Bondia anayefuata
nyayo za aliyekuwa bingwa wa dunia katika uzani wa middleweight Floyd
Mayweather, Gervonta Davis ametetea taji lake la uzani wa Super
Featherweight kwa kumuangusha Muingereza Liam Walsh katika raundi ya
tatu ya pigano hilo lililoandaliwa katika ukumbi wa Copper Box Arena.
Walsh mwenye umri wa miaka 31 aliinuka lakini konde jingine la mkono wa kushoto kutoka kwa Davis mwenye umri wa miaka 22 lilimlazimu refa Michael Alexander kuingilia kati na kusimamisha pigano hilo.
Davis ambaye anakuzwa na Floyd Mayweather sasa hajashindwa katika mechi 18.
Hivi majuzi alimshinda kwa njia ya knockout bingwa katika uzani huo Jose Pedraza.
SHARE
No comments:
Post a Comment