Mkuu wa wilaya ya Kilolo, Asia Abdalah akitazama mpira unaotumiwa na wanafunzi wa shule ya msingi Mlowa kata ya Mahenge
Na Matukio DaimaBlog
KUTOKANA na wanafunzi wa kiume na wa kike kutumia kiwanja
kimoja kibovu kwa ajili ya michezo shuleni hapo ,serikali ya wilaya
ya Kilolo mkoani Iringa imeiagiza kamati ya shule ya msingi Mlowa
kata ya Mahenge kuhakikisha inatengeneza viwanja vya michezo kwa
wanafunzi.
Agizo hilo limetolewa na mkuu wa
wilaya ya Kilolo Asia Abdalah jana wakati wa ziara yake ya kukagua
miundombinu ya shule za msingi zilizopo kata ya Mahenge .
Mkuu
huyo wa wilaya alifikia hatua hiyo baada ya kushuhudia
wanafunzi wakicheza katika kiwanja hicho kibovu ambacho kina vichaka
katikati na wanafunzi hao kukosa vifaa vya michezo ,kuwa akiwa mkuu
wa wilaya hiyo hajapendezwa kuona shule hiyo haina hata kiwanja
kimoja cha michezo .
" Naomba kuwaagiza
kamati ya shule kushughulikia kero ya viwanja vya michezo katika
shule hii maana wanafunzi wanahaki ya kuwa na vifaa vya michezo
vikiwemo viwanja vyenye sifa za michezo "
Hivyo
alimtaka diwani wa kata hiyo Shera Ngailo akiwa kama mwenyekiti wa
kamati ya maendeleo ya kata hiyo kusimamia utengenezaji wa viwanja
vyenye vipimo vya michezo kwa kushirikiana na kamati ya shule
hiyo.
Mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo
Malick Wilson alisema kuwa tatizo kubwa lililopelekea shule hiyo
kukosa uwanja wa michezo ni kutokana na eneo hilo kuzungukwa na
milima pamoja na mawe mengi japo alisema eneo la kutosha uwanja
mmoja wa michezo lipo ila lipo juu ya mlima.
Afisa
mtendaji wa kijiji cha Mahenge MUrady Nchimbi na diwani wa kata ya
Mahenge Shera Ngailo walisema wataanza mchakato wa kutafuta wadau
kwa ajili ya kushughulikia kero ya uwanja wa michezo shuleni hapo .
Wanafunzi
wasichana na wavulana katika shule hiyo wamekuwa wakilazimika
kutumia uwanja mmoja na mpira mmoja kucheza pamoja mpira wa miguu
ama mpira wa mikono kutokana na uhaba wa vifaa vya michezo .
|
No comments:
Post a Comment