Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Fabian Manoza(Mwenye kofia
ya njano akitoa maelezo kwa Wakuu wa Mikoa ya Kanda ya Magharibi
inayolima pamba ya Simiyu, Shinyanga, Geita, Mwanza, Kagera, Kigoma,
Singida na Tabora walipotembelea mashamba ya uzalishaji wa mbegu bora ya
pamba(UKM08) katika kata ya Mwabusalu wilayani humo.
Mkuu
wa Mkoa wa Singida, Mhe.Dkt.Rehema Nchimbi (wa pili kushoto) akichangia
jambo wakati wa ziara ya wakuu wa mikoa ya Kanda ya Magharibi inayolima
pamba walipotembelea mashamba ya uzalishaji wa mbegu bora ya
pamba(UKM08) katika kata ya Mwabusalu wilayani Meatu.
Mkuu
wa Mkoa wa Tabora, Mhe.Aggrey Mwanri (wa pili kushoto) akichangia jambo
wakati wa ziara ya wakuu wa mikoa ya Kanda ya Magharibi inayolima pamba
walipotembelea mashamba ya uzalishaji wa mbegu bora ya pamba(UKM08)
katika kata ya Mwabusalu wilayani Meatu.
Mkurugenzi
wa Bodi ya Pamba, Marco Mtunga akitoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali kwa
wakuu wa mikoa ya Kanda ya Magharibi inayolima pamba walipotembelea
mashamba ya uzalishaji wa mbegu bora ya pamba(UKM08) katika kata ya
Mwabusalu wilayani Meatu.
Mkuu
wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali Ezekiel Kyunga akiwasalimia wananchi
wa Kata ya Mwabusalu wakati wa ziara ya Wakuu wa Mikoa ya Kanda ya
Magharibi inayolima pamba walipotembelea mashamba ya uzalishaji wa
mbegu bora ya pamba(UKM08) ya katika kata hiyo wilayani Meatu.
Mkuu
wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Salum Kijuu akisalimiana na baadhi ya
viongozi wa Wilaya ya Meatu wakati wa ziara ya Wakuu wa Mikoa ya Kanda
ya Magharibi inayolima pamba walipotembelea mashamba ya uzalishaji wa
mbegu bora ya pamba(UKM08) ya katika kata ya Mwabusalu wilayani Meatu.
Bw.Charles
Thobias Mkulima kutoka kata ya Mwabusalu ambaye ametumia mbegu bora ya
pamba ya (UKM08) akitoa maelezo kwa Wakuu wa Mikoa ya Kanda ya Magharibi
inayolima pamba ambayo ni Simiyu, Shinyanga, Geita, Mwanza, Kagera,
Kigoma, Singida na Tabora walipotembelea mashamba ya uzalishaji wa mbegu
bora ya pamba(UKM08) katika kata hiyo wilayani Meatu.
Na Stella Kalinga, Simiyu.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Fabian Manoza amesema
Matumizi ya Mbegu bora na Kilimo cha Mkataba ni suluhu ya wakulima wa
pamba inayoweza kuwasaidia kuongeza uzalishaji.
Manoza
ameyasema wakati akitoa taarifa ya Wilaya ya Meatu kuhusu kilimo cha
Pamba kwa Wakuu wa Mikoa nane ya Kanda ya Magharibi inayolima pamba
waliotembelea eneo hilo kutoka Simiyu, Shinyanga, Geita, Mwanza, Kagera,
Kigoma, Singida na Tabora katika ziara yao kuona mashamba ya uzalishaji
wa mbegu bora ya pamba(UKM08) katika kata ya Mwabusalu wilayani Meatu.
Amesema
kupitia kilimo cha mkataba wananchi watakuwa na uhakika wa kupata
pembejeo bora za kilimo zikiwemo mbegu bora, mbolea na viuadudu kutoka
kwa watu au makampuni yatakayoweka mikataba nao.
“Tunatarajia
kuongeza uzalishaji ili kupata kata nyingi zaidi, tumewasisitiza
wananchi kuwa kilimo hiki cha mbegu bora lazima kiendane na kilimo cha
mikataba, wale wanaohitaji kununua pamba lazima waingie mikataba na
wakulima ili wapate faida walizokuwa hawazipati; baadhi yao wamekuwa
wakihangaika hawana uwezo wa kununua mbegu, viuadudu na kuhudumia
mashamba, lakini wakiingia mikataba hao watakaonunua pamba watatoa
huduma zote hizo kwa wakulima” alisema.
Ameongeza
kuwa pamoja na kilimo cha mkataba na matumizi ya mbegu bora ili
kuboresha uzalishaji wa pamba Wataalam wa Kilimo wanapaswa kuwapa
wakulima huduma zote muhimu za ugani ili wazingatie taratibu
Mkuu
wa Mkoa wa Geita, Mhe. Meja Jenerali Ezekiel Kyunga ameitaka Bodi ya
Pamba nchini kuboresha utaratibu wa kilimo cha mkataba ili kiweze
kuwanufaisha wakulima badala ya kuwakatisha tamaa.
Naye
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe.Aggrey Mwanri amesema ni vema Bodi ya Pamba
ikaweka utaratibu utakaowawezesha wakulima kupata mbolea na zana bora
za kilimo kwa mkopo ambao watarejesha baada ya mavuno.
Mkurugenzi
wa Bodi ya Pamba, Marco Mtunga amesema wakulima wa pamba kwa miaka ya
nyuma wamekuwa wanakumbana na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa
mbegu bora na kutopanda kwa kuzingatia mistari, hivyo katika msimu wa
mwaka 2017 jumla ya tani 8000 za mbegu bora zitazalishwa kwa ajili ya
kusambaza kwa wakulima na jitihada zinaendelea kufanywa kupitia kilimo
cha mkataba kuhamasisisha wakulima kulima kwa kuzingatia ushauri wa
wataalamu.
Aidha,
Mtunga amesema ili kuongeza uzalishaji wa pamba wakulima wahamasishwe
kulima kilimo cha mkataba na ili kilimo cha mkataba kiwe na tija kwao
Bodi hiyo inaendelea kutimiza wajibu wake kusimamia masharti yaliyowekwa
katika utekelezaji wa mikataba hiyo kati ya wachambuzi na wakulima wa
pamba.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe.Dkt.Rehema Nchimbi amesisitiza
kuwepo kwa mikakati ya kilimo cha umwagiliaji katika zao la pamba
ikiwepo uchimbaji wa mabwawa makubwa yatakayowasaidia wakulima wakati
wote badala ya kutegemea mvua tu.
Naye
Bw.Charles Thobias Mkulima wa kata ya Mwabusalu ambaye ametumia mbegu
bora ya pamba ya (UKM08) amesema mbegu hiyo imekuwa mkombozi kwa
wakulima kwa kuwa kulingana na mazao yalivyo sasa shambani, mavuno
yataongezeka kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na msimu uliopita.
Utekelezaji
wa Mpango wa uzalishaji wa Mbegu bora katika kata ya Mwabusalu Wilaya
ya Meatu Mkoani Simiyu umehusisha jumla ya wakulima 1,709 katika vijiji
vinne ambao kwa pamoja wameweza kulima jumla ya ekari 6,506 na
unafadhiliwa na Programu ya Kuendeleza Kilimo cha Pamba chini ya
usimamizi wa Bodi ya Pamba.
SHARE
No comments:
Post a Comment