KAMATI Kuu ya Act Wazalendo imemuidhinisha Ndugu Dorothy
Jonas Semu (pichani), kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa chama cha ACT Wazalendo.
Kabla ya uteuzi huu Ndugu Dorothy Semu amewahi kushika
nafasi za ukatibu wa Kamati za Sera, Mipango na Utafiti na Kamati ya Fedha na
Miradi.
Kwa mujibu wa Kiongozi wa ACT-Wazalendo Mhe. Zitto
Kabwe, kupitia ukurasa wake wa Facebook amesema, Ndugu Dorothy Semu ametoa
mchango mkubwa kwa chama hasa kwenye uandaaji
wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu, 2015 na masuala mengi ya kiutafiti juu ya sera na
mikakati ya Chama.
Ndugu Semu ni mtaalamu wa masuala ya Fiziotherapia
mwenye shahada mbili za eneo hilo kutoka Chuo Kikuu cha Western Cape, Afrika ya
Kusini.
Ana uzoefu wa zaidi ya miaka 16 wa kufanya kazi kwenye nafasi
mbalimbali serikalini na kwenye asasi za kiraia ikiwemo Mratibu wa kuzuia
ulemavu kwenye Programu ya Taifa ya Kupambana na Kifua Kikuu na Ukoma.
Tunamtakia kila la heri Ndugu Dorothy Semu kwenye
utekelezaji wa majukumu yake.
No comments:
Post a Comment