Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, ameondoka nchini leo kwenda Kigali
Rwanda, kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli, kwenye mkutano wa siku mbili wa “Transform Africa Summit 2017”.
Mkutano huo utawakutanisha
viongozi na wataalam mbalimbali Barani Afrika kwa lengo la kujadili
masuala kadhaa ikiwemo maendeleo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
(ICT), hususan katika Ukanda wa Afrika Mashariki.
Katika mkutano huo, Profesa
Mbarawa ataeleza kwa kina changamoto na mafanikio yaliyofikiwa na
Tanzania katika uwekezaji wa Miundombinu ya Habari na Mawasiliano,
Maendeleo ya Sera na Miongozo inayotumika hapa nchini katika kusimamia
sekta hiyo kwa lengo la kukuza uchumi wa nchi na kuiunganisha Tanzania
na Mataifa mengine.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
10 Mei, 2017
SHARE
No comments:
Post a Comment