TRA

TRA

Friday, May 26, 2017

EVEERTON KUCHEZA NA SIMBA AU YANGA,JULAI 13 UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


JS75712614
Timu ya Everton ya England yenye wachezaji nyota akiwemo Mbelgiji, Romelu Lukaku, itazuru Tanzania kucheza mechi za kujiandaa na msimu mpya wa 2017/18, tovuti ya klabu hiyo imeandika. Ziara hiyo ambayo itakuwa sehemu ya sherehe zao za udhamini mpya wa kampuni ya SportPesa, itaifikisha The Blues kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam unaomeza mashabiki 60,000 kucheza mechi Alhamisi ya Julai 13.  Everton itakuwa timu ya kwanza ya Ligi Kuu ya England daima kucheza mechi ukanda wa Afrika Mashariki – na itamenyana  na bingwa wa mashindano ya SportPesa Super Cup. 
Nchi mbili, Tanzania na Kenya zitakutanisha timu zao nane, nne kutoka kila upande katika michuano hiyo, kuwania nafasi ya kucheza na kikosi cha Ronald Koeman.    Mapema mwezi huu, Everton ilitangaza udhamini mnono wa rekodi na SportPesa wa miaka mitano na baada ya hapo kampuni hiyo ikaingia Afrika Mashariki kufunga ndoa na klabu kadhaa kubwa, zikiwemo SImba na Yanga. Michuano ya SportPesa Super Cup inatarajiwa kuanza Juni 5 hadi 11 mjini Dar es Salaam, ikishirikisha timu za Simba SC, Yanga SC, Singida United na Jang’ombe Boys za Tanzania, Gor Mahia, AFC Leopards, Nakuru All Stars na Tusker FC za Kenya. Bingwa wa michuano hiyo itakayofanyika Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam ndiye atamenyana na Everton.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger