Huddersfield walimaliza nafasi ya tano katika ligi ya Championship
Klabu ya Huddersfield Town
imepandishwa daraja kucheza Ligi ya Premia kwa mara ya kwanza baada ya
kulaza Reading 4-3 kupitia mikwaju ya penalti uwanjani Wembley Jumatatu.
Reading walimaliza nafasi ya tatu kwenye jedwali ligi ya Championship, alama nne juu ya Huddersfield
Christopher Schindler aliwashindia Town baada ya mkwaju wa Liam Moore kupaa angani nao mpira wa Jordan Obita ukaokolewa na kipa Danny Ward.
Klabu hiyo ya Yorkshire Magharibi haijacheza soka ya ligi kuu tangu 1972.
Reading, waliomaliza alama nne na nafasi mbili juu ya Town waliokuwa nafasi ya tano katika ligi ya Championship sasa wameshindwa katika fainali ya muondoano ya kufuzu kwa EPL baada ya ligi kwa mara ya nne.
CHANZO: BBC
SHARE










No comments:
Post a Comment