TRA

TRA

Monday, May 29, 2017

Barcelona: Ernesto Valverde ateuliwa kuwa meneja

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !
 Ernesto Valverde amekuwa mkufunzi mkuu wa Athletic Bilbao kwa miaka minne

Barcelona wamemteua Ernesto Valverde kuwa mkufunzi wao mkuu kwa mkataba wa miaka miwili, ambapo anaweza akaongezewa mwaka mwingine wa tatu.

Valverde ni mshambuliaji wa zamani wa Barca na alitangaza wiki iliyopita kwamba angeacha kazi Athletic Bilbao baada ya kuwaongoza kwa miaka minne.

Anachukua nafasi ya Luis Enrique aliyetangaza Machi kwamba angeihama klabu hiyo iliyomaliza nafasi ya pili La Liga msimu huu.
Anaondoka baada ya kumaliza mkataba wake wa miaka mitatu.
Enrique aliongoza Barcelona kushinda mataji matatu makuu msimu wake wa kwanza, mataji mawili makuu ya nyumbani mwaka 2016 na Kombe la Mfalme au Copa del Rey mwaka huu.

Walilaza Alaves 3-1 mechi yake ya mwisho kuwa kwenye usukani katika fainali ya Kombe la Mfalme Jumapili.

Rais wa Barca Josep Maria Bartomeu alimsifu Valverde, 53, kwa uwezo wake, ufahamu, ujuzi na busara na kusema: 

"Huwa anaendeleza wachezaji chipukizi na hucheza mtindo wa Barca." Valverde atazinduliwa rasmi kama meneja wa Barca Alhamisi.

CHANZO: BBC

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger