MUIMBAJI wa Kundi la Jahazi Modern Taarab, Leyla Rashid,
amefunguka kuwa tangu mumewe Mzee Yusuf aache kuimba Muziki wa Taarab,
amekuwa hana mzuka kama zamani zaidi ya kutamani na yeye amrudie Mungu
kama mumewe.
Leyla aliiambia Showbiz Xtra kuwa
tangu mumewe aache kuimba na kumrudia Mungu amekuwa hana mzuka kivile
wa kuimba na anatamani kumfuata mumewe ingawa bado anafikiria.
“Ukweli
naimba tu lakini sina munkari kama zamani hasa baada ya mume wangu
kujitoa kwenye kundi na kumrudia muumba, sijaacha rasmi kuimba ila
nafikiria zaidi kumfuata mume wangu katika kumtumika Mwenyezi Mungu,”
alisema.
SHARE










No comments:
Post a Comment