Wakulima wadogo nchini Tanzania hivi karibuni wataweza kupata taarifa
mbalimbali za kijiditali kuhusu masuala ya pembejeo, ukiwemo ushauri
utakaosaidia kutatua matatizo yanayowakabili kama vile upatikanaji wa
fedha, pembejeo na mafunzo.
Mradi
huo umezinduliwa na taasisi tatu za Alliance for a Green Revolution in
Africa (AGRA), Positive International Limited (PIL), na Grameen
Foundation katika sherehe zilizohudhuriwa na maofisa wa serikali,
wawakilishi wa vyama vya wakulima, taasisi za fedha, kampuni za mbegu,
wafanyabiashara wa nyenzo za kilimo na wale wanaojishughulisha na
biashara za mazao ya sekta ya kilimo.
Kifaa
hicho cha dijitali kitawawezesha wakulima kulipia mapema pembejeo
wanazohitaji kupitia simu za mkononi kwa bei nafuu. Pia kifaa hicho
kitawapa wakulima pembejeo kulingana na mazao na malengo yao ya
uzalishaji na pia kupata taarifa za ushauri kuhusu matumizi bora ya
pembejeo hizo.
“Moja
ya changamoto kubwa zinazowakabili wakulima ni kwamba hukosa fedha
mwanzoni mwa msimu wa upandaji mazao, jambo ambalo huwalazimisha
kutafuta fedha hizo kwa ajili ya ununuzi wa pembejeo na hivyo
kuwaongezea mzigo,” alisema Hedwig Siewertsen, kiongozi anayeshughulikia
masuala ya fedha wa shirika la Alliance for a Green Revolution in
Africa (AGRA).
“Kifaa
hicho cha dijitali kwa ajili kusaidia upatikanaji pembejeo za kilimo ni
ufumbuzi wa kipekee. Kitawaimarisha na kuwasaidia wakulima kutenga
fedha kwenye akaunti zao za simu ili waweze kununua pembejeo bora kwa
muda muafaka na kwa bei nafuu ya asilimia 30.”
Wakulima
wadogo nchini Tanzania huzalisha asimia 70 ya chakula ingawa karibu
nusu yao hawazalishi chakula cha kutosha kwa ajili ya mauzo.
Wanakabiliwa na ukosefu wa teknolojia ya kilimo cha kisasa, hawana uwezo
wa kujipatia pembejeo bora na wanakosa huduma za kiufundi za ughani
zinazoweza kuwasidia kukuza kilimo pamoja na ukosefu wa mafunzo. Mwakilishi wa AGRA nchini, Bw. Vianey Rweyendela akifafanua jambo wakati wa uzinduzi huo.
Badala
yake wakulima hawa wanategemea zaidi kilimo cha mvua, zana duni za
kilimo na mbegu hafifu ambazo ubora wake hupungua kila msimu wa kilimo.
Isitoshe,
wakulima wanaotaka kuwekeza katika kilimo cha kisasa wanashindwa kupata
mikopo kwenye taasisi za fedha kwa vile ni asilimia 6 tu ya mikopo ya
benki ndio imetengwa kusaidia sekta ya kilimo. Wakulima wanatumia fedha
zao chache kununua pembejeo za kilimo kutoka kwa walanguzi; pembejeo
ambazo mara nyingi hazina uthibitisho wa ubora.
Wakati
huo huo, wafanyabiashara wa pembejeo za kilimo wa sekta binafsi
wamegundua kwamba usambazaji wa huduma bora maeneo ya vijijini una faida
ndogo kutokana na gharama kubwa za kufanya biashara hiyo, uwezo mdogo
wa kifedha kwa upande wa wakulima na umaskini uliokithiri miongoni mwa
wananchi wengi vijijini.
Matokeo
yake ni kwamba wastani wa uzalishaji wa mazao mengi kwa hekta
unakadiriwa kuwa ni tani 1.7 na kwamba mavuno ya mazao muhimu ya chakula
kama vile mahindi yamekuwa yakipungua kwa sababu ya uharibifu wa ardhi
na hali mbaya ya hewa. Jinsi ya kupeleka kifaa cha dijitali kwa wakulima
Kifaa cha dijitali kitakuwa na mpango mahsusi wa mazao utakaowawezesha
wakulima kupata pembejeo kwa kuzingatia malengo yao ya uzalishaji.
Pia,
kupitia simu za mkononi, kitawezesha upatikanaji wa huduma za ughani kwa
njia ya ujumbe (SMS) kuwaelimisha wakulima matumizi ya pembejeo. AGRA,
shirika linaloongozwa na Waafrika wenye weledi wa kuwasaidia wakulima
wadogo barani Afrika, ndilo linalogharimia ukuzaji wa kifaa hicho cha
dijitali kupitia ufadhili wa MasterCard Foundation.
Taasisi
ya Grameen Foundation, ambayo ni taasisi inayojitegemea inayotumia
teknolojia ya dijitali kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya umaskini, ndio
inasisimia ukuzaji wa chombo hicho cha dijitali. Kifaa hicho pamoja na
huduma zake kitatolewa na kampuni ya pembejeo za kilimo ya Positive
International Limited, ambayo nembo yake ya kibiashara ya Snow Brand
imesaidia sana kutafuta ufumbuzi wa matatizo yanayowakabili wakulima
nchini Tanzania.
Mfumo huo wa ununuzi wa pembejeo utazingatia uwepo wa huduma za fedha za simu za mkononi zinazokua kwa kasi nchini Tanzania.
Uzinduzi ukifanywa na Mkuu wa AGRA nchini Bw. Vianey Rweyendela (wa
pili kulia) kwa kushirikiana na wawakilishi wa Positive International
Limited (PIL), na Grameen Foundation.
Mradi
huo utatekelezwa kwa kipindi cha miezi kumi na nane, ikiwemo awamu ya
miezi sita ya utafiti na maendeleo, na miezi kumi na mbili ya awamu ya
majaribio ya kifaa hicho cha dijitali. Majaribio yataanza na wateja 15
wa kampuni ya Positive International na wakulima wadogo 15,000 wa mikoa
ya Arusha na Mbeya.
Mazao
yatakayohusika katika mradi huo ni mahindi na maharage, ambayo ni muhimu
sana katika maeneo hayo. Kwa mfano, mkoani Arusha – moja ya maeneo
yanayohusika katika mradi – mazao hayo mawili hulimwa katika eneo la
hekta 150,000 ingawa kuna pengo la mavuno la asimilia 213 kwa upande wa
mahindi na asilimia 152 kwa upande wa maharage.
Matumizi
ya pembejeo bora ndio njia pekee itakayosaidia kuongeza mavuno kwa
asilimia 150 ili kutosheleza mahitaji ya chakula katika ngazi ya kaya na
pia kukuza mapato. Mkurugenzi Mtendaji wa Positive International, Karan
Kapoor, anasema soko la matumizi ya kifaa cha dijitali kwa mauzo ya
pembejeo za kilimo nchini Tanzania ni kubwa.
“Mamilioni
ya wakulima wadogo Tanzania wanahitaji upatikanaji wa pembejeo bora za
kilimo kwa bei nafuu. Tutaanza matumizi ya kifaa hiki cha dijitali kwa
kuwahusisha wafanyabiashara 15 kwa kipindi cha miezi 18 ijayo. Lengo
litakuwa kuwafikia wakulima 15,000 ili kuthibitisha matumizi endelevu ya
kifaa hicho.” “Baada ya hapo, tumepanga kupanua matumizi yake ili
kuwafikia wafanyabiashara 500 nchini bila ya kuwepo miundombinu mpya.”
“Watanzania
milioni 19 wanaishi kwa kutegemea mashamba madogo ingawa mtu mmoja kati
ya watu 25 hupata huduma ya umeme na watu wengi hawana maji safi na
salama majumbani mwao,” anasema Raphael Wolf, Meneja Mradi wa Grameen
Foundation.
“Kifaa
hiki kitaleta mapinduzi makubwa ya dijitali mashambani. Kwa mara ya
kwanza, wakulima wengi wataweza kupata raslimali wanazohitaji kuongeza
uzalishaji na mapato yao.” Jinsi wakulima wanavyopata pembejeo muhimu za
kilimo kama vile mbolea na kuongeza mavuno yao, shirika la AGRA
litapata fursa ya kutumia uwepo wa ubia wake na vitega uchumi vilivyopo
Tanzania kuwaunganisha wakulima na masoko kupitia ushirikiano na
wanunuzi wa kimataifa, wawezeshaji wa biashara na mashirika yasiyokuwa
ya kiserikali yanayoshughulika na upatikanaji wa masoko.
Mradi
huu ukifanikiwa Tanzania, washirika wake wanakusudia kutumia uwezo wao
wa pamoja kuanzisha dhana hii na kifaa hicho cha dijitali katika nchi
nyingine za Afrika, ukiwemo mtandao wa wafanyabiashara za kilimo katika
nchi za Malawi, Msumbiji, Zambia na nchi nyingine katika bara hili.
SHARE
No comments:
Post a Comment