Kijana mdogo
ameuawa nchini Venezuela katika siku nyingine ya maandamano dhidi ya
Rais wa nchi hiyo Nicolas Maduro, maandamano ambayo kwa sasa
yanazorotesha uchumi wa taifa hilo.
Maandamano hayo yanatajwa kurudisha uchumi nyuma
Kijana mwenye umri wa miaka
17, Luis Alviarez alipigwa risasi kifuani katika maandamano ya upinzani
kwenye mji wa Guasimo, Mashariki mwa nchi hiyo.Wito umetolewa wa kufanyika kwa uchunguzi kuhusu mazingira ya mauaji hayo.
Pia kwenye jimbo la Tachira, wanaharakati wapinzani wa shirika la Foro penal wamesema zaidi ya watu 40 walikamatwa siku ya jumatatu .
Takriban watu 40 wameuawa tangu maandamano kuanza nchini humo majuma saba yaliyopita.
CHANZO: BBC
SHARE










No comments:
Post a Comment