Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amehoji sababu za polisi
kumshikilia mmiliki wa shule ya Lucky Vincent badala ya trafiki
waliokuwa barabarani siku ya ajali iliyoua watu 35.
Akiomba mwongozo wa Spika kuhusu jambo hilo leo, amesema katika eneo
husika kuna vizuizi vya ukaguzi vinne lakini trafiki hawakuona kuwa basi
hilo lilikuwa kimezidisha watoto na hawakuwa wamefunga mikanda.
Amesema badala ya trafiki hao kuchukuliwa hatua, anakamatwa mmiliki ambaye hakuwapo.
Akijibu mwongozo huo, Naibu Spika, Dk Tulia Ackson amesema suala hilo halijatokea bungeni.
SHARE
No comments:
Post a Comment