Msanii
wa muziki wa hip hop, Nikki wa Pili amefafanua kauli yake ya uchunguzi
ufanyike katika ajali iliyoua 32 Arusha baada ya kudai kuna baadhi ya watu wameshindwa kuielewa kauli yake hiyo.
Rapa
huyo amedai kuwa ni jambo la utu kama tatizo litajulikana na kufanyiwa
marekebisho kwa vitendo na siyo kuhukumu watu au kumtafuta mchawi nani kipindi
hiki, huku akitaka asinukuliwe vibaya.“Nasikitika watu wameninukuu
vibaya sana niliposema uchunguzi ufanyike wengine wameniponda lakini
sijachukia kwani hawajanielewa,” Nikki alikiambia kipindi cha Planet
Bongo cha EA Radio.
“Uchunguzi
ukifanyika sina maana ya kumhukumu mtu mmoja hapana bali tuweze
kujifunza. Watu wengi waliokusanyika uwanjani kuaga walimu na wanafunzi
wameonyesha utu lakini pasipo tukio hili kuchunguzwa utu wao utakua
hauna thaani kwani matatizo haya yatajirudia mara kwa mara,”Aliongeza,
“Inawezekana kuwa mikanda ilikosekana kwenye ‘bus’ walilokuwa wamepanda
wanafunzi na walimu wa Lucky Vicent Academy au mwendo haukuwa mzuri
lakini tatizo linaweza kuwa hali ya hewa hivi ni vitu ambavyo
vikifanyiwa uchunguzi vinaweza kutukumbusha tabia zetu na tutajifunza
wakati mwingine,”
Katika
hatua nyingine Nikki amewaona watu wanaoweka mitandaoni picha za ajali
na kusema kuwa ni vitendo vya udhalilishaji na kuongeza kwamba zipo njia
nyingi za kutoa taarifa kwenye mitandao lakini siyo kwa ku- ‘share’
picha za ajali ambazo watu wanakuwa wameumia vibaya.
SHARE
No comments:
Post a Comment