Madaktari watalii waliotoa msaada wa awali baada ya ajali iliyowaua
wanafunzi na waalimu wa Lucky Vicent Academy wameahidi kuwapatia msaada
majeruhi watatu waliobaki hospitalini hata kuwapeleka nje ya nchi kama
itahitajika.
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan
Akiwaongoza wakazi wa Arusha kuomboleza msiba katika viwanja vya
Sheikh Amri Abeid, Makamu wa Rais, Mh. Samia Suluhu amesema kwamba
Madaktari hao walikuwa watalii na gari lao lilikuwa mbele ya ‘bus’ la
wanafunzi na hata baada ya ajali kutokea wao ndio walikuwa watu wa
kwanza kutoa msaada wa kitaalamu.
Katika hotuba yake Makamu wa rais amesema kuwa hata baada ya kutoa
msaada watalii hao kutoka shirika la afya nchini Marekani wameahidi
kujitolea kuwapatia matibabu wanafunzi watatu ambao ni majeruhi wa ajali
hiyo na hata msaada kutoka nje ya nchi wapo tayari kututoa.
SHARE
No comments:
Post a Comment